Mwanao ana Usonji....! Utapoteza pesa kwa Waganga wa Kienyeji....!
Nina jirani yangu kahamia Mtaani hivi karibuni, ana Mtoto wa Kiume wa miaka 4 pia...! Mwanzoni nikasema Baba ake anamdekeza sana Mtoto...!
- Mtoto analia bila sababu.
- Ukimkataza kufanya Jambo hasikilizi.
- Hawezi kuongea, japo anaongea Maneno machache lakini sio kwa Usahihi.
- Hana marafiki.
- Ameanza Kusoma Vidudu, walimu wanasema japo Mtoto haongei ila Ana akili Shupeni, na pale Mwalimu anapofundisha, anakua wa Kwanza kumuelewa Mwalimu kuliko Watoto wengine Timamu.
Kuna siku naongea na Baba wa Mtoto ananambia Mwanae na Usonji, naujua Ugonjwa wa Usonji, na huwa una Daraja tofauti, kuna Watoto wanaonhea japo taratibu, na wengine wanakua hawawezi kuongea...!
Nilimshauri ampeleke Mtoto Hospital, akasema alishanya hivyo, kwa sasa hakuna Vidonge ama Madawa ambayo Mtoto atapewa Hospital ili aanze kuongea, ila kuna Wataalamu Wachache wana Clinic za Watoto wenye Usonji kuwasaidia kuongea na kuwaweka sawa...! Na gharama ni kubwa wana charge mpaka 400,000 kila mwezi.
Huyu Mzazi hawezi kumudu, anachofanya ni kusoma Mtandaoni mbinu mbalimbali za kumsaidia mtoto then anamfanyia Mwanae.
Mfano moja ya mbinu, anakaa na Mtoto kwa saa kama moja, hafu ana cheza Nyimbo za Bongo fleva kwenye simu yake, huku akijifanya kama Nyimbo imemkolea, akiweka na Vibe, na mwanae nae akawa anamfatisha Baba ake kwa kutikisa kichwa, ana play nyimbo zile zile kwa saa nzima, ni baada ya siku 3 tu, mtoto kuna nyimbo akawa amezipenda, hawezi kuongea lakini unaona anavyohangaika kuimba kama Bubu.... Leo ni mwezi wa pili namsikia akiimba nyimbo lakini kaanza kutamka maneno machache kwenye Nyimbo anazopenda...!
Tiba ya Usonji ni Vitendo zaidi, tumia Google, tafuta group za Whatsapp za Wazazi wenye Watoto wenye Usonji.....!
Baada ya mwaka tu, mwanao hatabaki alivyo leo.