Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Omba yasikukute kama haya, mkuu nakuonea huruma sana maana mtoto kiukweli anauma aisee pole sana.
 
Mtoto kapimwa hajawahi kuingiliwa kimwili... bado fumbo,
KAUPATA WAPI???
naam ndio maana nika mwambia aende kule "" kuna mkuu anaitwa deception alishawahi kusema kuwa HIV+ ni fake "" so akienda kule na kukutana na hoja zake atajuwa wapi pakuanzia....lakini bado nimeona kuna michango ya members wengi tu Humu ambayo inamashiko "" kuna ambao wamemwambia akapime DNA huwenda walibadilishiwa mtoto wakat alivyozaliwa" kuna ambao waliosema huwenda mtoto alitumia vifaa vilivyotumiwa na mtu aliyeathirika"" kama nyembe .sindano .neel cuter etc ambavyo vimepelekea kumsababishia maambukizi"" so huwenda hizi sababu tajwa zikawa na tija zaidi na kufumbua fumbo linalotukabili
 
Naandika huku natetemeka kwa huzuni na uchungu
naelewa jinsi mlivyo sasa hivi poleni sana wazazi, pole kwa baby darling, she is too young to suffer like that,
She needs you guys more than ever plz msimnyanyape wala ndugu zake wasimbague.

Ooh poor innocent soul, wish ningekua hapo nikampa tight hug.

Guess what big bro, the kid will be fine and healthy kama tu mkimuanzishia dozi ya majani ya mlonge na mbegu zake, Mlonge unapandisha cd4 haraka sana na hata kuponesha HIV kikubwa msiuache katika kila diet yake.

Nina ushuhuda wa Mlonge anza sasa utakuja kunambia.

Tengeneza unga wa lishe, utafanya asubuhi unampa kijiko cha chai cha unga wa majani ya mlonge changanya kwenye uji mpe anywe, jioni mpe unga wa mbegu za mlonge kijiko cha chai changanya kwa uji mpe anywe.

Utaleta mrejesho.
 
You are a real humble African mkuu...[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Mungu awatie nguv katika kipindi hiki kigum cha mpito[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Najua mtu kinga yako ya mwili ikishuka lazima magonjwa yakupate, kula healthy food tuone kama kutakua na kitu kama hicho.
So kwa asilimia kadhaa nakubaliana na Deception.

Suala la DNA siliafiki sababu watazidi kumuweka mtoto pabaya, what if majibu yakawa kweli sio wao je familia itaweza kua nae au ndio watampeleka kituo cha mayatima.

Hoja ya kuipata masaloon au kujichoma na vitu vya ncha kali katika michezo nakubaliana nalo.
 
katika kucheza na wenzake na kuumiana vitafunwa mbalimbali ndo kinaweza kuwa chanzo
 
poleni sana.

Possible kaupata kwa zile njia nyingine kama kutobolewa na kitu chenye ncha kilichotoka kwa mwenye maambukizi, saluni, Hospitalini n.k.

Hizo njia zina percent ndogo sana lakini haimaanishi mtu hapati maambukizi, wengi tume stick kwenye njia kuu ya maambukizi kwa njia ya ngono.
 
Hapo majibu ni mawili tu.
Maana ashasema.mtoto hajaingiliwa naona watu hawasomi habari yote wanaanza kukoment.
1.Moja ni kuwa MTOTO sio wako ulibadilishiwa hospital
2.walishare kitu chenye ncha huko shuleni na watoto wenzake.
MAANA SIONI SABABU NJE YA HIZO MBILI.
 
okay "" nimekuelewa ktika hizo hoja zote ulizoziwakilisha hapa "" dhidi ya huu mkasa uliopo mbele Yetu " kwakweli nimejikuta na muelewa zaidi deception "" na ningekuwa mimi ndiye mtoa mada "" ningejitahidi kumtafuta haraka ili aangalie namna yakuweza kulitatua hilo fumbo ""
 
Pole sana Ndugu! Mungu akufanyie wepesi na Kufikiri Vema!
 
Kuna kama hio ilitokea katika shule moja (jina kwenye mabano) ni case ya kweli na mimi nipo karibu na shule hio ya msingi ilitokea kisa kama hicho baada ya wazazi kushindwa kuelewa ameupataje huyo mtoto na ni bikra, mzazi alianza kumuuliza kwa umakini mtoto wake akamuuliza swali lingine je hamchanjani na viwembe shuleni? Binti akajibu Kuna rafiki yetu anasemaga ambaye yupo tayari nimchanje tubadilishane damu nampa kitoli (viazi mviringo vilivyowekwa rangi ya njano sisi huku tunaita binzali) baba mzazi akaenda shuleni akaonana na walimu akawaelezea case akaitwa mtuhumiwa wakamwita na mzazi wake, mzazi wake akasema ukweli kua kijana wao alizaliwa na vvu, aisee ilitia simanzi mtoto alipoulizwa kwann anafanya hivyo akasema tuumwe wote. Jamani tuwape tafadhari watoto wetu na ikiwezekana hao watoto watangazwe wazi kua wanamaambukizi ili wenzio wanzao wawe na tafadhari
 
Kaa na binti yako muulize taratibu bila hasira atakuambia ukweli hawezi pata hiv kirahis hivo kuna kitu kafanyiwa au ka share vifaa
 
Duuu pole sana
1.Shuleni
2.Kama kulikuwa na housegirl before
3.Wageni
4.Majirani
5.Watoto ktk michezo
6.Mazingira yanayo mzunguka.. Labda kakutana na kitu cha ncha Kali.
 
Utata unaonisumbua ni siku tutakayo mwambia ila mpaka sasa yeye hatujamwambia.

Huu ni mtihani huko mbeleni mkuu.
pole sana mkuu, wakati mwingine maisha yanakatisha tamaa.

Mi nna mtoto wa anko wangu kazaliwa nao mpaka leo ni mwaka wa 23 yuko vzr afya njema.

nahisi kaupata kwenye vifaa vya ncha kali na michezo ya mashuleni huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…