Mwanasayansi anasema dini ni ugonjwa wa akili

Ndo maana hupati kazi, na bado utakiona cha moto .


Sent using Jamii Forums mobile app
ni bora tu niamini mungu yupo
 
Fanya yote ila Nguvu ya Mungu haichunguziki, sema yeye kwa imani yake hatumwingilii ila isitufanye na sisi tuamini anachokiamini.
Kama hachunguziki... kwanin mnatupa habari zake?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Lakini huyo muumbaji sidhani kama anahitaji chochote kutoka kwa alivyoviumba....
Utaratibu wetu wa kuishi ulipaswa uende kwa kadri ya maarifa yetu... mfano ng'ombe hawezi kula majani kwa kutumia miguu yake...
Nature ndio determinant how we should live.... remember this life is all about surviving and nothing else....
ni bora tu niamini mungu yupo
 
Kuamini uwepo wa Mungu si tatizo ila umefundishwa kumwamini mungu yupi? Yule mkamilifu au yule mwenye sifa za kibinadamu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuamini uwepo wa Mungu si tatizo ila umefundishwa kumwamini mungu yupi? Yule mkamilifu au yule mwenye sifa za kibinadamu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo nakwambia mkuu, haya maisha its all about surviving, ukitaka kujua kwamba sisi sio wema njaa iongezeke alafu wawe wanajua kuna kiasi fulani cha msosi kwa jirani....hakuna ataekubali kustarve to death...
Kinachotutofautisha sisi na viumbe vingine ni maarifa na hivyo inatufanya tujitengenezee sheria na kanuni...ili tusidhulumiane kwa wale wababe.
Kama tungejitoa akili tukaamue tuishi tu kama wanyama porini basi wale wadhaifu ndio utakuwa mwisho wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jipya...hta neuroscientist mwenzie na father of psychodynamic Sigmund Freud akiegemea mawazo ya natural biologist Charles Darwin aliibuka na dhana hyo hyo...Lakini mwisho wa Maisha yake alimrudia Muumba wake.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaazi kweli kweli.
Wazungu na waarabu wametuingiza kwenye matatizo yao so sad.
Wao ndo waliahidiwa moto, wao ndo yaliwakuta majanga ya Sodom na Gomorrah, wao ndo walipata mafuriko ya safina sijui.
Cha ajab walipokuja Africa wakatuhusisha na shida zisizotuhusu maana hata mitume hatukuletewa kwa maana hatuhusiki.
 
Kila mtu anaweza kutafsiri dini ajuavyo na humu kuna makundi tofauti,ila kitu kimoja ni kwamba wanaosema dini ni upuuzi na wanaoona dini haina umuhimu au haina mahusiano na mungu hufanana kitu kimoja.

Wenye kuona dini ni upuuzi chimbuko lao kule wenye kuona dini si muhimu na haina mahusiano na mungu.

Kwahiyo utaona ni kwa jinsi gani ni rahisi kwao kusema dini ni upuuzi,na wengine hufika mbali hata kusema hakuna mungu
 
Ina maana ukristo na uislamu ulisambzwa afrika tu?
 
Ina maana ukristo na uislamu ulisambzwa afrika tu?
Habari ndo hiyo ...
Mfano sisi tulikuwa na dini zetu za Kiafrika, uliwahi kusikia wazungu wakiziabudu?
Kuna mambo yalikuwepo lakini hawa wageni walipokuja tukayaona ya kishenzi .... hadi leo kuna mambo mengi yanaendelea kupotea kabisa ...

Hata ukarimu wa kiafrika unapotea ghafla .... kupoteza kizuri ukapokea kibaya ni ugonjwa tu wa akili...
 
Kwahiyo huko Asia hakuna uislamu wala ukristo?

halafu nachojua waafrika tulikuwa na imani mbalimbali ambazo hadi Leo zipo na sidhani kama zilikuwa dini,na ndiyo maana kuna wana hizi dini lakini bado wana imani zile za kiafrika.
 
Kwahiyo huko Asia hakuna uislamu wala ukristo?

halafu nachojua waafrika tulikuwa na imani mbalimbali ambazo hadi Leo zipo na sidhani kama zilikuwa dini,na ndiyo maana kuna watu ni waumini wa hizi dini lakini bado wana imani zile za kiafrika.
 
Kwahiyo huko Asia hakuna uislamu wala ukristo?

halafu nachojua waafrika tulikuwa na imani mbalimbali ambazo hadi Leo zipo na sidhani kama zilikuwa dini,na ndiyo maana kuna wana hizi dini lakini bado wana imani zile za kiafrika.
Dini ni nini? na Imani ni nini?
 
Dini ni nini? na Imani ni nini?
Dini ni jamii ya watu wenye shauli moja...Imani ni kuzingatia na kukibeba kwa ukweli kile wanachokieneza kwa jamii nyingine isiyoamini wakiaminicho wao.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…