Sister Abigail
JF-Expert Member
- Sep 2, 2020
- 2,886
- 9,088
- Thread starter
- #41
Nahisi msando kuwa karibu na macelebrity ndo inapelekea mda fahamu zinamtoka anafanya mambo ya ovyo.Couple haihitaji kukubaliwa na mtu mwingine yeyote, inatakiwa kujikubali yenyewe tu.
Hivi Lulu akimwambia Msando kwamba Msando ana wivu wa kisenge, anataka Lulu aachwe ili Msando aolewe na Majizo, atie timu kwenye "mjengo" Msando atajisikiaje?
Kuna maneno mengine mwanamme hata kama unaona hii couple haidumu, hutakiwi kusema hilo.
Unajuaje wanaridhishana vipi wakiwq wawili mpaka uanze kuongea habari za kuachana?
Msando ni kama mtu aliyepewa nyundo halafu tatizo lolote anataka kulimaliza kwa nyundo.
Hata akiwashwa pumbu atataka kujipiga nyundo.
Si kila kitu kinahitaji ushauri wa kisheria.
Zaidi, mwanasheria kutoa ushauri wa kisheria kwa mtu ambaye si mteja wako, hajakuomba ushauri na hakulipi, tena mitandaoni, ni ushamba na ulimbukeni.
Yani hapo Msando anaweza kuanzisha ugomvi mpya kati ya Lulu na mmewe, Lulu akasema kumbe wewe umefanya makusudi kujenga kabla hujanioa ili nyumba iwe kwa jina lako peke yako, tukiachana uniache bila nyumba.
Wakati inawezekana hata mume hakuwa na nia hiyo, alitaka kujenga kabla ya kuoa kama sehemu ya utamaduni wa makabila mengi wa mwanamme kuwa na kwake kabla ya kuoa.
Kuna vineno vineno vingine vidogo tu, lakini vinainesha uwezo wa mtu wa kufikiri.
Inawezekana watu wakawa hawana mpango wa kuqchana, maneno ya mtu yakapanda mbegu ya kuachana, mbegu ikastawi na kuchanua maua vizuri.
Maneno yanaumba, tujihadhari na maneno yetu.
Watu wameoana juzi tayari kashaanza kumtajia mke mgao wa Mali hii ni kama kumpa taarifa indirect kwamba "mtaachana tu"