Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Doctor Kilangiee!! nakupinga sasa hatuwezi kuuza nchi kwa ajili ya makaratasi sasa!!!!!!

1. Umezungumzia suala la common heritage kuwa kwa kuwa baadhi ya nchi hazina madini basi iwe ruksa kwenda kuchota kwenye nchi zilizonayo .........Haikubalikiii!!!!! madini ni yetu na suala la madini si kama kwenye "high sea" amabapo kila mtu anaruhusiwa kutembea na kuvua ( shammba la bibi ) @ " RESCOMUNIIS"

2.Eti tutaenda kunyolewa bila maji huko ICSID kwa ku breach 'fair and equitable treatment' Hakuna hiyooo!!! wao wametutendea equity gani mpaka na sisi tuwatendee equity wanatuibia halafu waseme equity " IF YOU NEED EQUITY DO EQUITY:

3. Kwa kuwa hakuna mkataba wa kimataifa ambayo haina claus ya " PACTA SUNT SERVANDA" na kwa kuwa hao "mabwana wakubwa" hawakuiheshimu na wakaendelea kusafirisha mchanga kwa udanganyifu " maana yake hawajaheshimu mkataba" basi automatical doctine ya '' REBUS SIC STANTIBUS '' ita apply na kuufanya huo mkataba usitekelezeke !! yaani umevunyika nganganyanga beyond repair.
 
Uchunguzi wa upande mmoja hauwezi kukubalika katika mahakama za kimataifa na hili ndio kosa kubwa tulilolifanya.

Kingine cha kushangaza ni kwanini serikali haitaki kukubali hoja ya ACASIA ya kuunda Tume Huru kuchunguza jambo hili?
 

Wenzako wanachambua mambo kitalaam wewe unaleta ushabiki na ufia chama.
 
Uchunguzi wa upande mmoja hauwezi kukubalika katika mahakama za kimataifa na hili ndio kosa kubwa tulilolifanya.

Kingine cha kushangaza ni kwanini serikali haitaki kukubali hoja ya ACASIA ya kuunda Tume Huru kuchunguza jambo hili?
Hiyo tume huru kutoka wapi???? hivi mnaongea tuu!!! tume huru ni hii ya kwetu zaidi ya hapo ukileta vya nje ya nchi yoote ni mazungu usidhani watawaangusha wenzao....ukileta wa nchi za kiafrika hasa ghana , south africa, na kenya hao watu wanaofanya nao kazi migoni wanawajua,,,, wanajifanya wao ni wazungu weusi na watakwenda upande wa mzungu au ni rahisi kununuliwa,,,,,, unafikiri watakubali kuiacha bilioni 300?
 
Sasa tutegemee nini? au ndio tutulie mambo yatapita kama kawaida.
 
Ila mwisho wa siku tukikubali kufuata kila kilichopo kwenye makaratasi, tusitarajie kunufaika kupitia madini yetu kwa mwavuli wa fair and equity int'l treats.

Hata kama ikiundwa tume mpya itakayo husisha pande zote za mkataba, mzungu atacheza rafu tu.

Labda tukomalie kwenye udanganyifu wa kiwango na uwiano wa madini kwenye hivyo vifusi, lakini hofu yangu ni nani atapuliza kipyenga?
 
FUPI TAMU,NDEFU INAKERA....
summary kidogo jamani
FUPI TAMU,NDEFU INAKERA....
summary kidogo jamani
Jamani tupo bize sasa na teminology za international law of contract kwa maslahi ya taifa hivyo tunatarajia kila anayeshika keybord atakuja na manenono kama REBUS SIC STANTIBUS, EX EAQUO ET BONO n.k , hivyo kama mtu hayajui madude haya atulie ajifunze. Tumesemwa sana mara ooh bongo hatujui sheria za mikataba sasa tulieni turarue rarue kabisa.
 

Mkuu,ni kweli kabla ya kuanza vita ilitakiwa kuanza kwa kupanga vikosi vyetu pamoja na dhana zitakazotumika kwa kuangalia uwezo wa zana za wenzetu ( sheria,taratibu,mikataba kama alivyoandika Dr.)ndipo sasa tungeingia vitani kifua mbele tukiwa na uhakika wa ushindi kutokana na kujua adui yetu yukoje.

Sasa vita imeanza ndio wakina "General Mayunga,Black Mamba & wababe wengine wa vita hii" wanaanza kutoa mbinu zao ambazo mpaka sasa majeshi yetu yalipofikia, tukisema tuwarudishe nyuma ndio tujipange twaweza rushiwa likombora tukaangamizwa,na tukisema tuendelee mbele na mapambano, hizo zana zetu pengine hazifai tena kwa mapigano ya huko mbele.

Sasa tuache mihemuko,tukae kama Taifa tuwe na mjadala mpana ili tufikie hatima iliyo salama kwa ustawi wa vizazi na vizazi vya Taifa letu.
 
huu wako sio uzalendo bali ni uzwazwa.

Ukweli unauma. Mkuu punguza hasira.

Hata hivyo kuna kanuni ya Kiutawala inayosema ni bora kufanya uamuzi hata kama uamuzi huo ni mbaya. Kwani ukiwa mbaya utasahihishwa kuliko kukaa kimya wakati unajua kitu hicho siyo siyo sahihi.

Hii ni vita hivyo tukubali kutakuwa na maumivu. Inawezekana tukashindwa hivyo kulipa fidia, sawa tu ila tutarekebisha baadhi ya mambo ambayo ni wizi dhahiri. Kama kweli mchanga huo hauna faida kiasi hicho mbona wanapiga kelele na kukimbilia mahakamani! Wanajua walivyokuwa wanafaidi na sasa povu linawatoka.

Cha msingi waletwe wachunguzi wengine kuthibitisha uchunguzi uliofanywa na Tume halafu walipe fedha zote walizotuibia. Kisha mikataba ifanyiwe review
 
Ndio maana Nyerere alikataa tusichimbe madini sasa nyie mkaingia kichwa kichwa kwenye haya mamikataba na masheria ya kinyonyaji kuhusu rasilimali zetu na haya sasa ndio matokeo yake.
 
Wananchi wetu wanaangalia tu kama muvi! Wanacheka, wanalia, wanashangilia na wanabet! Yote kwa yote, kila mtu anatabiri hili picha kwa namna yake, hasa kwa kuegemea ktk mwisho anaoutaka yeye!

Binafsi nimemuelewa doctor-Loud and Clear!
 
Hahaha have a nice day
 
Ah Kumbe wewe ni graduate wa Jana tuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Mnatusumbua humu tunadhani mmegraduate miaka 20 hivi nyuma

Issue siyo kugraduate bali IQ yake iko katika nafasi gani,kama IQ yake ni kubwa kuliko wewe lazima akusumbue tu
 
Mkuu hiki Ni kitu ambacho hata Mimi najiuliza sipati jibu kabisa.
 
Ndio maana Nyerere alikataa tusichimbe madini sasa nyie mkaingia kichwa kichwa kwenye haya mamikataba na masheria ya kinyonyaji kuhusu rasilimali zetu na haya sasa ndio matokeo yake.
Huko awali hatukuwa tomesoma mambo haya na wala hatukushirikishwa vema kama wanasheria nchi ilikuwa bado changa sasa tumebibea tunaichanilia mbali na kuondoa ugandamizi wa kila aina uliomo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…