Nimesoma makala iliyo andikwa hapo awali na ambae sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule kwa mtazamo wangu aliongea akiwa "open minded" kama ataendelea kuwa "open minded" anaweza kuisadia Serikali kufungua/kuendesha Kesi za Jinai na Madai zenye mantiki sio kukidhi matakwa ya Kisiasa au mhemeko wa Kijamii. Uhenda hata walioondoka walikuwa "hawawezi kufunguka" juu ya uhalali wa mustakabali wa baadhi ya Kesi ambazo ama waliziendesha kwa dhana ya "bora liende" au kwa kupima "busara ya Mahakama" au "kutimiza matakwa" ya wafanya maamuzi.
Kwa nafasi hii kubwa inahitaji weledi Mkubwa sana kutumika katika kulinda maslahi ya Nchi, Wananchi na Viongozi wa Nchi. Busara hii ijumuishe pia uwezo wa kusema " HAPANA" pale ambapo mazingira yote ya Kitaaluma yanaonyesha jibu ni Hapana, yamkini usisieme NDIO ili kulinda Mkate wako wa siku.