Mwanasheria Dkt. Nshala Rugemeleza: Mkataba wa bandari ni wa kiuhaini, Umevunja katiba ya nchi na utakwenda kuvunja sheria za nchi

Mwanasheria Dkt. Nshala Rugemeleza: Mkataba wa bandari ni wa kiuhaini, Umevunja katiba ya nchi na utakwenda kuvunja sheria za nchi

Huyo ana PhD ya investment law kutoka Harvard ametoa hoja zake,haya nawewe jitambulishe elimu yako halafu jibu hoja tuone nani anaonekana mjuaji hapa.
Na wewe je? Una PhD ya wapi? Au bendera tu?!!!

Kila mmoja anachukua na kuziamini hoja za upande anaoutaka inavyoonekana, km n hivyo basi endelea kushabikia huko ulikoamini......simple!
 
Hakuna mkataba kwa sababu yaliyomo hayakidhi matakwa ya mkataba
 
"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa,kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA,this is nonsense,itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna...
Huyu ndio mwanasheria sasa sio yule AG.
 
"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa,kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA,this is nonsense,itategemea vipi HGA wakati IGA ...
Kwanini serikali isiwe inaomba ushauri kwa vichwa kama hivi vya Wazalendo kama mwanasheria Rugemeleza kupitia mkataba kabla ya kusaini?

Wapeni wazalendo kama huyu mkataba wa LNG waupitie kabla hamtuingiza kilenge na Kule pia.
 
Huwezi kuomba ushauri kwa watu independent kama malengo yako ni kuuza nchi
 
Hawa waimba taarabu wametupiga tena!
mchana kweupe
Macho yana cheka Moyo unaliaaa
Macho yanacheka mimi moyo unalia
Nikimkumbuka wangu maridhia
Nikimkumbuka wangu maridhia
Chozi hunitoka kwa zake tabia
Chozi hunitoka mimi kwa zake tabia
Nenda nateseka nalia nalia nendateseka mimi nalia nalia
Siku zitafika kukugeukia, Siku zitafika kukugeukia
Waja hangaika, uliyenambia
Waja hangaika wee ulienambia
hivi kweli bandari zetu zinaondoka? historia inajirudia aliyewalinda watumwa ni mwafrika mwenzao na wanaotutesa ni watanganyika wenzetu wameamua kutudhalilisha kwa hali ya juu itafika wakati tunaweza kuona aibu tukienda nchi za watu kuitwa Watangayika.
natamani watu wakubali sasa imetosha!
 
Na wewe je? Una PhD ya wapi? Au bendera tu?!!!

Kila mmoja anachukua na kuziamini hoja za upande anaoutaka inavyoonekana, km n hivyo basi endelea kushabikia huko ulikoamini......simple!
Haya weka hoja za upande unaoamini tuzione hapa,acha maneno mengi
 
Job Ndugai tumnyonge ila haki yake apewe, hii mikataba ya kizezeta aliijua mapema, sema mdomo ulimponza.

Leo ndo naelewa Kwa Nini akina Msukuma walimwijia juu Kwa kuvujisha uozo...

Hapo vip!!

Hili sakata la bandari limewachukiza watanganyika wengi sana kwa asilimia 99..wananchi wengi wanaumia mioyo wanavumilia tu..ila ni sawa na kumpiga mtu makofi mwenye nguvu nyingi kuliko wewe ila amefungwa kamba mikono.

Sasa kwa utafiti wangu mdogo ni fursa kwa vyama vya upinzani na wanaharakati mbali wanaipenda nchi kuweza kuleta mabadiliko.

Wanachi kwa sasa ni sawa na maji yanayotaka kuvunja ukuta yaweze kutembea,na ukuta huu unata katobo kadogo tu then yenyewe yatamaliza kuangusha ukuta.
 
Back
Top Bottom