Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 673
- 865
Nashukuru sana kwa kutuwekea hii nyaraka. Yaani hapo nimesoma na nimeelewa ishu ni nini.Yuleyule aliyefanya figisu hadi kumfutia Leseni mwanadada Fatuma Karume, Mwanasheria mkuu wa Serikali bwana Feleshi amempeleka Wakili msomi ndugu Mwabukusi kwenye Kamati ya maadili ya Mawakili.
Katika malalamiko yake Mwanasheria wa Serikali anasema eti:
1. Mwabukuzi ni mchochezi.
2. Mwabukusi kavunja maadili ya uwakili kwa kuongea na vyombo vya habari baada ya ya kesi na kutoa matamshi ya kutaka Spika, Mbarawa na Waziri mkuu waachie ngazi.
3. Kwamba Mwabukuzi kaivunjia heshima mahakama.
Namkumbusha Mwanasheria mkuu kuwa asitafute diversion, kashindwa kuitetea serikali kwenye suala hili la mkataba sasa asianze witchhunt ili kuwatoa wananchi katika reli.
Pia Mwabukusi naye kama Mtanzania analindwa na katiba kwenye haki ya kutoa maoni. Kama hizo kanuni zenu za uwakili vinavunja haki hii ya Wakili kutoa maoni yasiyovunja sheria basi hivyo vitu na NULL and VOID ABNITIO.
Kitu kingine, Kamati ya mawakili siyo mahakama. Kama Mwabukusi kavunja sheria, Mpeleke mahakamani. Katiba inasema Mahakama ndiyo chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki nchini.
Kwa hiyo ndugu Feleshi, unajidhihirisha tu kuwa Umeshindwa kuitetea serikali kwenye mkataba mbovu, sasa unafanya Witchhunt. Yote hii ili mnyamazishe wananchi ili mfanikiwe azma yenu ya Kugawa Bandari zetu na kuuza nchi!
Wananchi hatutokubali!
Barua yenyewe ya mwanasheria mkuu wa serikali hii hapa.
View attachment 2704399
View attachment 2704644
Pia soma: Wakili Boniface Mwabukusi amjibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, asema wakitaka wachukue hata vyeti vya shule ya msingi
Huyo Mwabukusi na yeye naona ana chengachenga kichwani kwa kugeuza Mahakama uwanja wa siasa badala ya uwanja wa haki kwa mujibu wa sheria.
Nilimsikiliza siku ile anatoa hotuba yake kuhusu Chifu Mangungo nikawa natikisa kichwa tu kwamba huyu jamaa na yeye ana matatizo kidogo.
Haiwezekani kesi bado inaendelea Mahakamani, na Mahakama haijatoa hukumu bado wewe unatangaza hukumu yako kwenye vyombo vya habari.
Huko ni kudharau mahakama na kujaribu kuidhalilisha ili ikitokea mahakama imetoa hukumu tofauti na yako, basi mahakama ionekane chenga mbele ya umma.
Ni vizuri kwamba serikali imeliona hilo na kuchukua hatua sahihi ya kumshtaki katika Kamati ya Maadili ya Mawakili.