Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World

Nashukuru sana kwa kutuwekea hii nyaraka. Yaani hapo nimesoma na nimeelewa ishu ni nini.

Huyo Mwabukusi na yeye naona ana chengachenga kichwani kwa kugeuza Mahakama uwanja wa siasa badala ya uwanja wa haki kwa mujibu wa sheria.

Nilimsikiliza siku ile anatoa hotuba yake kuhusu Chifu Mangungo nikawa natikisa kichwa tu kwamba huyu jamaa na yeye ana matatizo kidogo.

Haiwezekani kesi bado inaendelea Mahakamani, na Mahakama haijatoa hukumu bado wewe unatangaza hukumu yako kwenye vyombo vya habari.

Huko ni kudharau mahakama na kujaribu kuidhalilisha ili ikitokea mahakama imetoa hukumu tofauti na yako, basi mahakama ionekane chenga mbele ya umma.

Ni vizuri kwamba serikali imeliona hilo na kuchukua hatua sahihi ya kumshtaki katika Kamati ya Maadili ya Mawakili.
 
ni kweli kwamba zipo kanuni. lkn mbn kama vile una,ngmzia upande 1 uloshika mpini!? unasahau kwamba Tz imeshindwa kesi nyng xana na kutulazmisha kulipia hasara hizo kw kutotumia uadilifu wa hao wanasheria wanaotuwaklisha ktk kusaini hiyo mikstaba!!!
 
Si angalianza na Tundu Lisu kumfuta uwakili. Tundu Lisu matamshi yake kuhusiana na viongozi wakuu wa serikali ni makali zaidi ya huyu Mwabukusi au yale ya Fatuma. Au anaogopa muziki wa Tundu Lisu.
 
Watu wa hovyo kama huyu mwanasheria anae shindwa kila siku ndio Mh Rais ana wapenda maana wana kula mema ya nchi. Feleshi niko na mashaka na taaluma yake.
Hivi ile scandal yake ya makubaliano imeishia wapi?
 
Taifa lina safar ndefu sana kufika kwenye maziwa na asali:
Yani wanasheria walioingia mkataba ya ATCL,Ujenzi wa Kituo cha DART kwenye mafuriko Jangwani, Waliouza misitu na mashirika wanapandishwa vyeo alafu wanaotetea resilimali ndio wanafutiwa uwakili?

#Not yetu Uhuru.
#Mwingereza aliwahi kuondoka, angebaki tu.
 
Watu wa hovyo kama huyu mwanasheria anae shindwa kila siku ndio Mh Rais ana wapenda maana wana kula mema ya nchi. Feleshi niko na mashaka na taaluma yake.
Hivi ile scandal yake ya makubaliano imeishia wapi?
SAsa tuliruhusu vipi wakoloni waondoke? huoni kosa ni letu kungangania uhuru wakati tu watumwa kuliko hata uhuru tunaohisi tunao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…