Mwanasheria Mkuu wa Serikali kaamua kujikalia kimya kuhusu suala la Bandari?

Hivi kama nia ni njema na inalenga kukuza ustawi wa nchi na Wananchi wanaona hawako tayari kunufaika na hiyo deal Je,Kuna ugumu gani kuachana na hiyo deal? Kama kuachana na Mkataba huo ili tujipange upya inawezekana nadhani kunahaja ya kufanya hivyo.

Isijekuwa mkataba ulifika sehemu ambaya hali itakayo pelekea ukivunjika wanase NDEGE zetu.

Mimi naona ni Muhimu kusogeza mbele ili tufanye upembuzi yakinifu.
 
Money talk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkataba ulipofikia hatuwezi kuuvunja, maana bora tuendelee na Mkataba ili kuepuka kulipa ma gharama ya kuvunja Mkataba!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
AG hana sababu ya kuwaelewesha watu wenye comprehension disorder. Hata wakielekezwa na malaika watabisha tu. Hawa wataelewa wakiona matunda kama enzi za NBC, NMB, KIA nk. Maza ashike hapo hapo.
NBC ipi hiyo unayosema? Sikuizi wanauza Vocha/float tu, tembelea mikoani uone, usidanganyike na matawi mawili au matatu ya Dar, huko mikoani wako hoi, mfanyakazi ana miaka 15kazini bado anaenda na bodaboda hiyo nayo ni benki? NBC hana tofauti na TTCL kiuchumi, by the way mara ya mwisho NBC wametangaza ajira ilikuwa lini? lini umesikia wafungua tawi jipya? Hata wilayani hawapo.
 
Angekuwa mwadilifu angebwaga manyanga tu ijulikane
 
Kwa hili namtetea maana siku hizi pale bungeni yaani ndani ya Ukumbi wa Bunge, namaanisha wakati Bunge linaendelea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mheshimiwa TULIA ACKSON MWANSASU. Kama huamini angalia Mabishano wakati Halima Mdee akichangia Nani alistahili kusimama kumchallenge ni Tulia au Eliezer?
 
Inaonekana haku husishwa lakini ndege zetu zikishikwa wata muhusisha na sisi tutahusishwa kwani tutasaidia kulipa hilo deni
 
Kwani huyo mwanasheria mkuu wa serikali alipata division gani kwenye mtihani wake wa form four???
Mleta mada katumia tafsidi kuonyesha kwamba mtu akiwa na ueledi mfano wa shule maamuzi yake Yana kuwa na ueledi tofauti na mfano mtu wa cheti feki. Ile dhamana uliobeba katika ueledi wako. Inakuzuia kutenda kinacho kwenda kinyume na ueledi wako.
 
Kwa kawaida, AG ndio husimama Bungeni(tena ikibidi mara kwa mara) kutetea vifungu vya kisheria vinavyotiliwa mashaka au kupingwa na wabunge, ila katika hili, Spika na Wabunge wake ndio walisimama kama AG. Ajabu sana!!
Duh!
 
Salary Slip! Wewe ulitaka aongee nini! Ambacho wewe hukijui! Acha upuuzi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…