Ngandema Bwila
JF-Expert Member
- Sep 8, 2010
- 1,017
- 258
Dah! Mambo mengine ni magumu sana kuyaelewa, huyu ndiye mshauri mkuu wa sheria wa rais na serikali ya znz. Nauliza tu kwa anaejua, kauli yake si ndiyo kauli ya serikali ya znz?
huyu ndiye mtaalamu na mwenye uoni mkubwa wa namna maslahi ya zanzibar yalivyominywa kwenye katiba. kw aahiyo ni ajabau km wazanzibar wa kawaida ambao wanamwani huyu kuwasaidia kubaini mapungufu katika haya mambo ya muungano wataacha kumfuata. Yeye ndiye anaangaliwa. na kura yake ni msumari wa mwisho kenye jeneza la katiba mptya ya CCM. Chochote watakachokifanya sasa hivi ni kuingiza zanzibar kwenye machafuko ambayo hayakuwahi kutoke tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Wazanzibar wameshazungumza, waheshimiwe.
wapi lizaboni na simiyu yetu.....mibukusaba iliyo na akili kama mizombi.
Kakubali yote ya Tanganyika ila yote yanayoigusa zanzibar hataki...hata mambo yaliyo kwenye hati ya muungano. Hana tofauti na aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado,
Mungu awabariki wote wanaopiga kura za hapana,hao ndiyo mashujaa wetu. Hongereni makamanda muipendao nchi yetu,kura za hapana ndiyo mpango mzima. HAPANA,HAPANA,HAPANA Kuanzia bungeni mpaka mitaani, Warioba naungana naye kwamba tutakutana mtaani na hapo ndiyo watatujua kuwa hatupendi unafki.
zipi
Amekataa Ibara za 2,9,86,70 hadi 75, 128, 129,158,159,160,161,243 hadi 251 pamoja na nyongeza ya kwanza, maudhui yake hayo hapa:
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
9. Ukuu na utii wa Katiba
70. Muundo wa Muungano
71. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi
72. Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
73. Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano
74. Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
75. Wajibu wa viongozi wakuu kulinda Muungano
86. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais
128. Madaraka ya kutunga Sheria
129. Utaratibu wa kubadilisha Katiba
158. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mamlaka yake
159. Rais wa Zanzibar na mamlaka yake
160. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na kazi zake
161. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
243. Misingi ya matumizi ya fedha za umma
244. Akaunti ya Fedha ya Pamoja
245. Tume ya Pamoja ya Fedha
246. Mfuko Mkuu wa Hazina
247. Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina
248. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina
249. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali kuanza kutumika
250. Mfuko wa Matumizi ya Dharura
251. Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina
Nyongeza ya Kwanza: Mambo 14 ya Muungano
Upo sawa ndio maana hata yule alieomba mwongozo nimemshangaa sana
Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya JMT imekataliwa, hilo ndo hitimisho. Katiba inayopendekezwa kwa mrengo mwingine haitakubalika kisheria.