Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aikataa Katiba

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aikataa Katiba

Dah! Mambo mengine ni magumu sana kuyaelewa, huyu ndiye mshauri mkuu wa sheria wa rais na serikali ya znz. Nauliza tu kwa anaejua, kauli yake si ndiyo kauli ya serikali ya znz?

Kwa SITTA hilo ni somo gumu sana, Eti kadai kura haipigwi kwa vyeo. Enzi za mwalimu Huyo mwanansheria na Shen wato wangepata Msukosuko! Maana Kauli ya mwanasheria ni ya serikali, Kama vile pinda alivyo funika kombe jana kuhusu mahakama ya kadhi hiyo ni kauli ya serikali!
 
Tena wamelikoroga zaidi kwa kumtukana maana wameongeza makali kwenye msumari. Huyu mzee aliyepewa ruhusa kumtukana anadhubutu kusema "huyu jamaa anajifanya mjuaji na msomi" kwani huo ni uongo? Ni kweli ni msomi na mjuaji wa sheria na ndiyo maana akaaminiwa kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar siyo haya makenge yetu ya akina Werema na mwenzie mstaafu mzee wa vijisenti
huyu ndiye mtaalamu na mwenye uoni mkubwa wa namna maslahi ya zanzibar yalivyominywa kwenye katiba. kw aahiyo ni ajabau km wazanzibar wa kawaida ambao wanamwani huyu kuwasaidia kubaini mapungufu katika haya mambo ya muungano wataacha kumfuata. Yeye ndiye anaangaliwa. na kura yake ni msumari wa mwisho kenye jeneza la katiba mptya ya CCM. Chochote watakachokifanya sasa hivi ni kuingiza zanzibar kwenye machafuko ambayo hayakuwahi kutoke tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Wazanzibar wameshazungumza, waheshimiwe.
 
Walio piga kura za hapana ndio wazarendo wa kweli. haki ya katiba itapatikana kupitia hao.
 
Sitta anafanya maigizo.Akilini kajaza matope tuu..Hajui kuwa yote haya yataisha ijumaa na baada ya hapo atakuwa anajifungia tu ndani?
Stupid Samuel Sitta!
 
Huyu si mwanasiasa ni mwanasheria huwezi kumzihaki na kumchezea anavotaka 6i kama mzee wetu Warioba alivyo
 
Kakubali yote ya Tanganyika ila yote yanayoigusa zanzibar hataki...hata mambo yaliyo kwenye hati ya muungano. Hana tofauti na aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado,

nashukuru kwa ibara ulizoziweka hapo juu, nimezipitia mara kadhaa kujiridhisha na chaguo lake kalifanyaje, inaonekana hakufanya kwa kubahatisha na ana ujumbe wa wazi kuhusu mambo ya Muungano ndani ya katiba.
 
zipi
Amekataa Ibara za 2,9,86,70 hadi 75, 128, 129,158,159,160,161,243 hadi 251 pamoja na nyongeza ya kwanza, maudhui yake hayo hapa:
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

9. Ukuu na utii wa Katiba
70. Muundo wa Muungano
71. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi
72. Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
73. Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano
74. Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
75. Wajibu wa viongozi wakuu kulinda Muungano

86. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais

128. Madaraka ya kutunga Sheria
129. Utaratibu wa kubadilisha Katiba

158. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mamlaka yake

159. Rais wa Zanzibar na mamlaka yake

160. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na kazi zake

161. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

243. Misingi ya matumizi ya fedha za umma
244. Akaunti ya Fedha ya Pamoja
245. Tume ya Pamoja ya Fedha
246. Mfuko Mkuu wa Hazina
247. Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina

248. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina
249. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali kuanza kutumika
250. Mfuko wa Matumizi ya Dharura
251. Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina

Nyongeza ya Kwanza: Mambo 14 ya Muungano
 
Mungu awabariki wote wanaopiga kura za hapana,hao ndiyo mashujaa wetu. Hongereni makamanda muipendao nchi yetu,kura za hapana ndiyo mpango mzima. HAPANA,HAPANA,HAPANA Kuanzia bungeni mpaka mitaani, Warioba naungana naye kwamba tutakutana mtaani na hapo ndiyo watatujua kuwa hatupendi unafki.

Ni kweli ni mashujaa wetu lakini mabilioni ya kodi zetu yamekwisha teketezwa na hili kundi. Can we use Hon. Mwiguli Nchema Hansard on whether BMLK to continue or not to prosecute Hon. Sitta?
 
Wassira ameufyata !
Lukuvi ameufyata !
Kigwangwala ameufyata!
Na Sita ataufyata.
Tanganyika hoyeeee!
 
sita mbona unajidhalilisha sana...??!!
kwa maslahi ya nani
huogopi moto wa mungu?
 
huo ndio msimamo wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar kwani mwanasheria ni mteuzi wa raisi
 
Mungu amuongoze kuitetea Tanzania
 
Kuna watu wengi km sitta wanachezea sana watz.....TUTAWASHUGHULIKIA KM WANAVYOSHUGHULIKIA TULIOWATUMA KUTUWAKILISHANA BADO MENGI YAJA ILI MRADI CCM INAPENDA DAMU IMWAGIKE KWA AJILI TU WABAKI MADARAKANI NA WALAZIMISHE MAONI YAO SIO MAONI YETU TULIOWAAJILI
 
Huyu ni mfano wa kuigwa na sio werema! Hongereni wazanzibar kwa kuwa na Ag anayejitambua!
 
zipi
Amekataa Ibara za 2,9,86,70 hadi 75, 128, 129,158,159,160,161,243 hadi 251 pamoja na nyongeza ya kwanza, maudhui yake hayo hapa:
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

9. Ukuu na utii wa Katiba
70. Muundo wa Muungano
71. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi
72. Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
73. Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya muungano
74. Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
75. Wajibu wa viongozi wakuu kulinda Muungano

86. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais

128. Madaraka ya kutunga Sheria
129. Utaratibu wa kubadilisha Katiba

158. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mamlaka yake

159. Rais wa Zanzibar na mamlaka yake

160. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na kazi zake

161. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

243. Misingi ya matumizi ya fedha za umma
244. Akaunti ya Fedha ya Pamoja
245. Tume ya Pamoja ya Fedha
246. Mfuko Mkuu wa Hazina
247. Masharti ya kutoa fedha za matumizi katika Mfuko Mkuu wa Hazina

248. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina
249. Utaratibu wa kuidhinisha matumizi ya fedha kabla ya sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali kuanza kutumika
250. Mfuko wa Matumizi ya Dharura
251. Mishahara ya baadhi ya watumishi kudhaminiwa na Mfuko Mkuu wa Hazina

Nyongeza ya Kwanza: Mambo 14 ya Muungano

Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya JMT imekataliwa, hilo ndo hitimisho. Katiba inayopendekezwa kwa mrengo mwingine haitakubalika kisheria.
 
Katiba inayopendekezwa kwa ajili ya JMT imekataliwa, hilo ndo hitimisho. Katiba inayopendekezwa kwa mrengo mwingine haitakubalika kisheria.

Cc Chabruma, MwanaDiwani Lizaboni na vibaraka wote wa Lumumba!!

Kama hamtaelewa uzito wa kura ya HAPANA ya mwanasheria wa Zanzibar basi ombeni ufafanuzi!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom