Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukimwangalia usoni utajua wazi pasina shaka kuwa yuko tayari kwa lolote na haterereki wala hayumbishwi na mawimbi aliyoyaona pale bungeni.Nimependa sana msimamo wake,ameonesha dhahiri ni msomi na mpambanaji wa kweli.Kwangu mimi ni Alama ya USHINDI kwa msimamo wake.Kaandika Historia yake ya kipekee.mejitambua na wala hataki laana ya vizani vyake vijavyo
Msimamo ni kitu cha msingi katika maisha sifa ziwe juu yake mwanasheria MKUU WA #ZANZIBAR . Yule babu anasimama anasema sijawahi kuzungumza leo nizungumze kisha anazungumza ujinga usioeleweka chamsingi ni kuheshimu msimamo na maamuzi ya kila
mmoja kwa nafasi yake.
Amekataa Ibara za 2,9,86,70 hadi 75, 128, 129,158,159,160,161,243 hadi 251 pamoja na nyongeza ya kwanza, maudhui yake hayo hapa:Nani anajua Mwanasheria huyo kakataa ibara zipi
Hivi punde akipiga kura baada ya kuja bungeni,amepiga kura ya Hapana kwa sura kadhaa na ibara kadhaa.
Baada ya kupiga kura ya Hapana,kuna mjumbe amesimama na kuomba muongozo ambapo amemshambulia kwa dhihaka na kejeli huku akiungwa mkono na wajumbe karibu wote wa CCM bara na wakisema hafai,mnafiki etc huku Sitta akionekana dhahiri kuruhusu vijembe hivyo na hatimae kahairisha bunge hadi Kesho.
Ikumbukwe kuwa Mwanasheria huyu wa Zanzibar alijiuzuru ujumbe wa kamati ya uandishi iliyo chini ya Chenge baada ya wajumbe wenzie kukataa mambo 17 aliyoyaleta ya Zanzibar yasiingie kwenye katiba ila bunge na kina Sitta walifanya siri.
Kakubali yote ya Tanganyika ila yote yanayoigusa zanzibar hataki...hata mambo yaliyo kwenye hati ya muungano. Hana tofauti na aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado,Kiukweli znz mwanasheria wanaye.ila huku kwa kina tumbili.tu mwizi!
Sasa hivi hawana ujanja ule, media kibao.. watetezi wa haki kibao hata ndani SMZ... Labda kumuweza wamuunganishe kwenye ile kesi ya ugaidi ya akina sheikh Farid na wenzake.kama kaletwa chini ya ulinzi mkali atakuwa kizuizini, yale yale ya abdul jumbe!
huyu ndiye mtaalamu na mwenye uoni mkubwa wa namna maslahi ya zanzibar yalivyominywa kwenye katiba. kw aahiyo ni ajabau km wazanzibar wa kawaida ambao wanamwani huyu kuwasaidia kubaini mapungufu katika haya mambo ya muungano wataacha kumfuata. Yeye ndiye anaangaliwa. na kura yake ni msumari wa mwisho kenye jeneza la katiba mptya ya CCM. Chochote watakachokifanya sasa hivi ni kuingiza zanzibar kwenye machafuko ambayo hayakuwahi kutoke tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Wazanzibar wameshazungumza, waheshimiwe.
Hii ni tetesi nimeipata kwamba ili akidi ipatikane,watu wenye nguo za kiraia walimfikisha na kuhakikisha ameingia, akidi inatafutwa! Natafuta taarifa zaidi,nina wasiwasi wajumbe wengine pia wanaweza kuletwa under the same style,mwenye uhakika zaidi afunguke au mwanasheria mwenyewe