MWANASHERIA, NKIKO AMUUA MPENZI WAKE CHANZO NI WIVU WA MAPENZI

MWANASHERIA, NKIKO AMUUA MPENZI WAKE CHANZO NI WIVU WA MAPENZI

Scott junior

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2022
Posts
3,705
Reaction score
5,540
Mwanasheria Keneth Nkiko (28) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake, Magreth Richard (22), mfanyabiashara na mkazi wa Manispaa ya Musoma akimtuhumu mpenzi wake huyo kuwa na mahusiano na wanaume wengine.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kupitia kwa Kamanda, Pius Lutumo limesema tukio hilo limetokea mnamo Oktoba 5, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mtaa wa Mwigobero, Manispaa ya Musomana kubainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Lutumo mtuhumiwa anadaiwa kumuua mpenziwe kwa kumpiga na kitu butu kichwani kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha yaliyosababisha dada huyo avuje damu nyingi na kufariki papo hapo

Inadaiwa mtuhumiwa alipata taarifa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa na tabia ya kuleta wanaume wengine ndani wakati ambapo yeye hakuwepo hatua iliyopelekea kutenda muuaji hayo kabla ya yeye mwenyewe kunywa sumu kwa lengo la kujiua lakini alikimbizwa hospitalini na kulazwa huku hali yake ikiendelea vizuri.

Aidha inaelezwa baada ya kutenda kosa hilo mtuhumiwa aliandika ujumbe na kuposti kwenye "WhatsApp Status' majira ya saa 3:26 asubuhi akiomba kusamehewa kwa kitendo hicho, ujumbe huo ulisomeka "Wale nilowakosea naomba mnisamehe Mungu nisamehe"

#KitengeUpdates
IMG_3981.jpeg
 
Death row inmate mwingine hata wiki haijaisha!
Nje ya mada: Sasa atakuja mtu hapa atasema marehemu alikuwa mchaga. 😊
 
Ngoja nasi tuanze sasa,maana naona mmeweka ni kamchezo Karede kutuua 🤒
 
Back
Top Bottom