Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Akihojiwa na chombo kimoja cha habari, Mwanasheria Phillipo Mwakilima anemkosoa vikali Spika Tulia Ackson kwa staili yake ya kujifanya ni mtafsiri sheria na mwalimu wa sheria kila sehemu anayokuwepo.
Wakili Mwakilima, akaponda kauli za spika kuwa eti bungeni walipitisha makubaliano na siyo mkataba wakati barua kutoka serikalini ya kuwasilisha mkataba ule bungeni ilitamka wazi kuwa serikali inataka bunge liridhie "Mkataba baina ya serikali na Dubai".
Pia Wakili Mwakilima akamkumbusha Spika kuwa hoja yake ya kusema kuwa katiba ya kufuata katika mambo ya nchi ni ya Kiingereza, Siyo kweli kwa sababu kwa mujibu wa muongozo wa sheria ya kutafsri katiba , Katiba rasmi ni ya KISWAHILI na si ya Kiingereza.
Wakili Mwakilima akamalizia kwa kusema kuwa huenda Tulia Ackson amemiss sana kufundisha darasani, kwa hiyo ni bora akarudi darasani kufundisha badala ya kudanganya na kupotosha watu huku nje.
Unaweza kutazama kipande cha Mahojiano hapa: