Mwanasheria wa tiGO katika Organogram ya Kampuni ni mtu mdogo sana, hawezi kuwa na access na mifumo yote aliyoitaja

Mwanasheria wa tiGO katika Organogram ya Kampuni ni mtu mdogo sana, hawezi kuwa na access na mifumo yote aliyoitaja

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Kampuni yoyote, hasa kampuni kubwa kama tiGO inakuwa na organization structure yake ambayo iko well organized. Mwanasheria sio part ya management bali ni muajiriwa wa kawaida tu ambaye kwa kawaida huwa wako chini ya Idara ya Rasilimali Watu.

Lazima wana departments kadhaa ambazo kila moja ina majukumu yake. Mwanasheria wa kampuni anakuwa chini ya Idara ya Rasilimali Watu ambayo lazima iwe na mkuu wake wa idara.

Pia kampuni lazima iwe na msemaji ambaye ndiye anahusika na kuisemea kampuni kwenye mambo yote yanayoihusu. Na yeye anakuwa yuko chini ya hiyohiyo idara ya rasilimali watu.

Masuala yote yanayotoka nje, hasa yanayohusu taarifa za wateja hayawezi kufanyika bila kupitia hii idara ya rasilimali watu. Maombi ya taarifa za wateja yakishamfikia mkuu wa idara ndipo yeye sasa atawapa maelekezo wahusika waandae nyaraka zinazotakiwa kulingana na request husika.

Huyu mwanasheria wa tiGO imekuwaje kila kitu amefanya yeye, mpaka saini amehusika yeye peke yake.

Ombi la taarifa za mteja amepokea yeye (ambapo zilitakiwa zifike kwanza kwa Director wa HR)
Print-out za KYC ametoa yeye (ambapo alitakiwa atoe mtu wa Registration)
Print-out za tiGO pesa ametoa yeye (ambapo alitakiwa atoe mtu wa Mobile Money Transactions)
Barua ya majibu ameandika yeye (ambapo alitakiwa aandike Director wa HR)

Inawezekanaje mtu ambaye hayupo hata kwenye management ya kampuni anafanya mchakato wote yeye peke yake bila hata management kujua? Mpaka saini zote ni za kwake tuu, hamna za mkuu yeyote wa kitengo chochote. Hii ni ajabu sana.

Kamwe kwenye kampuni kubwa kama MIC haiwezekani mwanasheria uwe na access ya kila kitu, haiwezekani mwanasheria unakuwa na access na mifumo yoooote. Sasa mwanasheria akifanya kazi za watu wa IT na watu wa IT watakuwa na kazi gani?

Screenshot_20211103-092909.jpg
 
Mimi naona kubwa pale ilikuwa kuithibitishia Mahakama kuwa Mbowe alituma fedha Tshs. 500,000 kwa mtuhumiwa lakini kwa kawaida kuna kosa gani kumtumia mtu fedha kama rafiki, mtu mnayefahamiana naye au mtu mwenye shida.
 
Tatizo hapa tigo's local management yenyewe ndiyo iko chini ya MFUMO! (ndiyo modus operndi ya fbi yetu) Kwahiyo labda kuna mtu alijisahau.

Vinginevyo wakili wao HASWA siyo huyu, na asingetumiwa na tanpol kirahisi namna hii.
 
Mimi naona kubwa pale ilikuwa kuithibitishia Mahakama kuwa Mbowe alituma fedha Tshs. 500,000 kwa mtuhumiwa lakini kwa kawaida kuna kosa gani kumtumia mtu fedha kama rafiki, mtu mnayefahamiana naye au mtu mwenye shida.

Umejisumbua walau kujua aliyetumiwa pesa ni nani?
 
Mimi naona kubwa pale ilikuwa kuithibitishia Mahakama kuwa Mbowe alituma fedha Tshs. 500,000 kwa mtuhumiwa lakini kwa kawaida kuna kosa gani kumtumia mtu fedha kama rafiki, mtu mnayefahamiana naye au mtu mwenye shida.
Uko sahihi mkuu. Ukiachilia mbali namna maombi ya taarifa yalivofika kwake/Tigo - shahidi alikuwa na wajibu wa kuonesha tu kuwa namba aliyopewa kuitolea taarifa ilifanya hivo kwa namba za washitakiwa. Matokeo yake akatoa taarifa za miezi miwili zikionesha taarifa za watu wengine wengi pia.

Watu hao hawajalindwa taarifa zao japo hawahusiki na kesi hii. Mpaka shahidi anamaliza ushahidi hakutamka kwa mdomo wake kuwa kulikuwa na miamala iliyoenda kwa washitakiwa (labda documents zitaonesha). Badala yake ameacha maswali mengi sana ambayo yanaibua hoja kuhusu ushiriki wake katika jambo zima.

Sikuwahi kusikia kampuni ya kibiashara ikiwa na mfumo unaoruhusu mawasiliano yake na nje/umma yakiwa mikononi mwa jmtu ambaye hayuko kwenye management. Tena mashirika mengi yanazuia wafanyakazi wake hata kutoa comment yoyote kuhusu jambo la kampuni (ndio maana ya kuweka watu wa mawasiliano ya umma).

Shahidi anaulizwa kama katika viambatanisho kuna barua aliyopokea kutoka polisi, anajibu hapana. Kama barua ilikuwa minuted na uongozi wake wa juu kuonesha alipewa maelekezo kufanya aliyofanya, anajibu hapana. Je alishughulikia jambo hilo toka mwanzo mpaka mwisho peke yake, anajibu ndio.

Ameiacha tigo katika wakati mgumu na ingeweza kutokea kesi ndogo nyingine kuhusu jinsi ushahidi ulivopatikana - utetezi labda kwa makusudi uliacha tru jambo hili lipite!
 
Mimi naona kubwa pale ilikuwa kuithibitishia Mahakama kuwa Mbowe alituma fedha Tshs. 500,000 kwa mtuhumiwa lakini kwa kawaida kuna kosa gani kumtumia mtu fedha kama rafiki, mtu mnayefahamiana naye au mtu mwenye shida.
Hapa ndio unajiuliza arguement kama hizi zinasaidiaje Mbowe kutoka kitanzini. Kwa hiyo mtu kama muandishi wa habari, akipewa majukumu ya uafisa uhisiano, mtadai huyu ni muandishi tu. Hamuamini ndani ya taasisi kuna nafasi anapewa mtu anaejua sheria kuepuka kufanya makosa ya kisheria?
 
Na wewe mfungulie kesi ili tupate ukweli kati yake na wewe nani anasema ukweli.
 
Hapa ndio unajiuliza arguement kama hizi zinasaidiaje Mbowe kutoka kitanzini. Kwa hiyo mtu kama muandishi wa habari, akipewa majukumu ya uafisa uhisiano, mtadai huyu ni muandishi tu. Hamuamini ndani ya taasisi kuna nafasi anapewa mtu anaejua sheria kuepuka kufanya makosa ya kisheria?
Arguments kama hizi ndio zinatumika kupima ukweli au uwongo wa shahidi.

Arguments kama hizi ndio zinapelekea ushahidi wake kuwa na mashiko au kutokuwa na mashiko.

Arguments kama hizi ndio zitaeleza kama iwapo vielelezo vya ushahidi wake vichukuliwe na mahamaka au vipotezewe. N. K
 
Hapa ndio unajiuliza arguement kama hizi zinasaidiaje Mbowe kutoka kitanzini. Kwa hiyo mtu kama muandishi wa habari, akipewa majukumu ya uafisa uhisiano, mtadai huyu ni muandishi tu. Hamuamini ndani ya taasisi kuna nafasi anapewa mtu anaejua sheria kuepuka kufanya makosa ya kisheria?
Na watu wa aina yako ndio shida ya taifa hili. Sidhani umeelewa point ya jamaa. Shahidi ni legal officer (mshauri wa maswala ya sheria). Majukumu kwa sehemu kubwa ni hayo na kwa sehemu ndogo ni mengine. Usitake kuonesha kuwa ni yeye pia mtu wa Tigo pesa, au IT department! Point kubwa hapa ni kuwa ushahidi wake unaongeza mashaka kuliko kuyaondoa.

Mbowe katuma pesa. Hilo ndilo jambo alipaswa kulionesha na kama kutuma au kutumiwa sio kosa, hakupaswa kutoa taarifa hizo, kama amezitoa basi ushiriki wake lazima uhojiwe!! Mashaka yanayohojiwa ni kama alikuwa na mamlaka ya kufanya hivo na alifanywa kwa mujibu wa sheria.

Mbona mnakuwa viazi kiasi hiki, hukujua kulikuwa kuna kesi ndogo ya kupinga maelezo ya mshitakiwa kuletwa Mahakamani na hata kupinga hati ya mashtaka?? Jaji mmoja alikubaliana na waleta shauri kuwa hati haikuwa sawa na irekebishwe (alipaswa kuifuta kesi) na wa pili akaonesha hakuna ushahidi maelezo yalichukuliwa kwa mateso na vitisho. Unajua kuwa kesi ya pili utetezi ungeshinda ndio kesi nzima ingekosa "standing" na kufutwa kabisa?? Wasingefikia hata huku kwenye Mbowe kutuma pesa.

Nakushauri usiangalie mwisho wa jambo, sheria huangalia limefikiwaje.
 
Huyu mwanasheria wa tiGO imekuwaje kila kitu amefanya yeye, mpaka saini amehusika yeye peke yake.
hapo ndipo tunaposhangaa tulio wengi, hata Mahakama nayo ikabaki inashangaa - ombi la barua yeye, kusaka data za mteja yeye, kujibu na kusign barua yeye, hivi hawa TIGO kumbe ni taasisi ndogo namna hii, yaani ni sawa na haya makanisa yetu ya kilokole mitaani - kila kitu ni baba mchungaji... kama hayupo basi mnawekewa recorded voice clip.
 
Back
Top Bottom