Kingine kilichonishangaza ni kusema hakuna taarifa za aliyesajili line.
Hii maana yake hata wale matapeli wanaosumbua watu wanatumia mwanya huu kusajili line na kuibia watu kwa sababu taarifa zao hazitafahamika kuwa ni wapi na nani amewasajilia line zao.
Na kama sivyo, basi shahidi #5 alikusudia kuwachafua TIGO kwa makusudi ili kutimiza matakwa ya ushahidi wake bila kuathiri ukweli wa maelezo yake.
Nadhani ni wakati sasa wa wateja wa mitandao ya simu kuanza kubadili mtazamo juu ya sheria za faragha zinazomlinda mtumiaji wa huduma.
View attachment 1997073