Mwanasheria wa tiGO katika Organogram ya Kampuni ni mtu mdogo sana, hawezi kuwa na access na mifumo yote aliyoitaja

Sasa wewe thibitisha iwapo zile laki tano alizotuma Mbowe zilienda kweli kifadhiri ugaidi bila kuacha shaka yoyote.
 
Yaani, basi tu!
 
Mkuu, hadi sasa kesi ya utetezi bado haijaanza, kesi ipo hatua ya mashtaka. Kama jaji ataamua kuna kesi ya kujibu hapo ndio mtaanza kusikia wanajiteteaje.

Kinachofanyika sasa ni kudiscredit ushahidi wa upande wa serikali ili ikiwezekana, jaji aone mashtaka hayana mashiko, au washtakiwa hawana kesi ya kujibu.
 
Mkuu hapo kwenye Baba mchungaji nimebaki nacheka tuu [emoji1787]
 
Inaonekana huyu Avae Kapala Freddy kawa surprise sana acheni mambo yaende yafika mwisho atakayeokota mfupa au atakayeambulia harufu ajulikane maisha mengine yaendelee
 
Unamfundisha Mbuzi.
 
Kingine kilichonishangaza ni kusema hakuna taarifa za aliyesajili line.

Hii maana yake hata wale matapeli wanaosumbua watu wanatumia mwanya huu kusajili line na kuibia watu kwa sababu taarifa zao hazitafahamika kuwa ni wapi na nani amewasajilia line zao.
Na kama sivyo, basi shahidi #5 alikusudia kuwachafua TIGO kwa makusudi ili kutimiza matakwa ya ushahidi wake bila kuathiri ukweli wa maelezo yake.

Nadhani ni wakati sasa wa wateja wa mitandao ya simu kuanza kubadili mtazamo juu ya sheria za faragha zinazomlinda mtumiaji wa huduma.
 

Attachments

  • Screenshot_20211102-174010.jpg
    40.8 KB · Views: 1
Kwa style hii usishangae Laini yako ikafungwa wakaisajili juu kwa juu wanakomba pesa na kuifanyia uharifu
 
Kwa style hii usishangae Laini yako ikafungwa wakaisajili juu kwa juu wanakomba pesa na kuifanyia uharifu
Hakika mkuu unachokisema.

Niliwahi kusikia tetesi kuwa baadhi ya mawakala ukimpa kitambulisho kusajili anakutengenezea mazingira ya kuamini kuwa mtandao unasumbua ili akuchukue alama za vidole zaidi ya mara 1 kumbe anasajili line zingine mbali ya ile unayosajiliwa wewe.

Kwa majibu haya kuwa hawawajibiki kumlinda mteja kutoka kwa mwanasheria wa kampuni ni hatari zaidi.
 
kibatala aligusia pale kesi ya kibubu ya tigo mteja kuchukuliwa hela kwenye kibubu ,mi ni mpenzi wa kuweka hela tigo kibubu kwasababu hamna makato Ila nikahamisha benki fasta baada ya kumsikiliza kibatala

Halafu yule zezeta akasema hajui kama kampuni yake ina mgogoro huo....yaani Ni lezafea wa kiwango Cha lami
 
Huyu shahidi wa Tigo, anafikirisha na kutia mashaka sana. Kuna kila dalili kuwa huyu ni member wa genge la kutengeneza/kubumba kesi kwa watu tishio kwa CCM na Serikali (watawala)...

Hebu cheki majibu yake. Ni aidha ana KIBURI CHA UZIMA kwa sababu anawategemea watu fulani fulani watamlinda au alijibu swali hili bila kufikiria madhara yake kwake na kampuni...

SWALI LA WAKILI KIBATALA: Mlichukua hatua gani kumlinda mteja...?

JIBU LA SHAHIDI TIGO NI: Hiyo siyo kazi yetu. Hakuna hatua tuliyochukua kumlinda mteja...!!!

##Inasikitisha kuwa, hata majaji wote wanaosikiliza kesi hizi hushirikiana na upande wa mashitaka na mashahidi wao kutafuta mwanya wa kumtia hatiani na kumfunga mtuhumiwa....

##Ndo kusema, hata Jaji ni sehemu ya syndicate hii ya kuwafunga wanasiasa wakosoaji wa serikali na CCM.

Lakini, Mimi naona kabisa kuwa haya mambo yanaenda kwisha sasa na Tanzania kuzaliwa upya...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…