Mwanaume ajinyonga hadi kufa golini. Aacha chupi ya kike pembeni

Mwanaume ajinyonga hadi kufa golini. Aacha chupi ya kike pembeni

 
Ila siku hiv uhai umepungua thamani sana kwa baadhi ya watu yan kuua na kujiua imekuwa jambo la kawaida
Mwengine huyuView attachment 2087330
Screenshot_2022-01-18-18-50-01-1.jpg


Sent from my SAMSUNG-SM-G900A using JamiiForums mobile app
 
Tyson Kilasi (32), Mkazi wa Kijiji cha Mawindi Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe, amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwenye goli la kuchezea mpira wa miguu wa kijiji hicho huku pembeni akiwa ameacha nguo ya ndani ya kike.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mawindi Kata ya Igima, Elias Mwinami amethitibitisha kutokea kwa kifo cha Kijana huyo na kusema kifo hicho kimetokea usiku wa kuamkia January 18,2022.

Mwinami amesema chanzo cha kifo cha Kijana huyo bado hakijafahamika ambapo eneo ambalo mwili wa Kijana huyo wameukuta ni eneo la goli la mpira wa miguu na wamekuta nguo ya ndani ya Mwanamke.

“Tumemkuta ananing’inia kwenye goli lakini chanzo bado hakijafahamika na kimsingi tunalaani kitendo hiki ifike mahali tuelimike na hivi karibuni tu Poliai walikuja kutoa elimu kwa kweli wananchi waache kujichukulia sheria mkononi"
Ukiua mtu kwa kumtuhumu kwa kosa fulani, hapo utakuwa umejichukulia sheria mikononi. Lakini ukiamua kuutoa uhai wako kwa hiari yako mwenyewe bila kushurutishwa na mtu sijui tutasemaje kuhusu hili.
 
hapo wa kulaumiwa ni jinsia ya kike tu, lazima watakuwa ndio chanzo cha baharia kututoka. kama hajafumaniwa akaningínizwa na wakaweka chupi pembeni kama kutuma meseji, basi watakuwa walikuwa wanafanya yao hapo uwanjani walipomaliza wakagombana jamaa akaamua kujiningíniza. si unajua hao jamaa zamani walikuwa mkoa wa Iringa, bado ile asili yao ipo kwenye damu.
 
Back
Top Bottom