Mwanaume akikataa mimba au kukutelekezea mtoto, usitumie majina yake Kwa mtoto wako


Baba kakataa mimba.
Baba kakataa kulea mtoto.

Sasa kwa nini mtoto aitwe kwa Jina lake?
Sio ishu ya chuki ili ni ishu ya Haki na wajibu

Mtoto anaweza kuitwa majina yako na ukaishi naye na ukamhudumia na akakuchukia licha ya kuwa Mama yake hayupo
 
Hayajamkuta ndio maana anaona rahisi tu kuandika nadharia hapa jukwaani
Naam huyu bado huyu.
Unakuta familia inakukalia kikao, uamuzi unapita upotezwe kwa namna yoyote haswa ushirikina.
Aisee sitasahau maisha yangu yoote.
Na mpaka sasa,hata nikitaka kumuhudumia mtoto hawataki maana kuna mazingira wanayatengeneza nionekane nimemkataa na simtunzi mtotoo.
Sio kila familia ni ya kuoa
 
Mkuu io situation yako ndio naipitia wakati huu sasa yani ni matatizo sana adi mtu unawaza kumtelekeza tu akae na lifamilia lake huko kwasababu wanajidai kama wanaweza kulea nk mara ghafla wanalalamika utoe pesa then ghafla wana block namba zako ili ukiwatafuta uonekane mwenye shida na wajisikie raha unavyo hangaika sasa watu kama hawa mwanaume akiwapotezea atalaumiwa kweli yani adi mtu unashindwa kufanya kazi kwa ufanisi kisa wapumbavu wachache
 
Sasa mtu kama ww hata mtu akiongea unamuelewa kwa kuwa tayari ushapitia uhalisia.
Ndugu hapo ni kukaa kimya tuu liwalo na liwe mtoto akikua atakutafuta tuu.
Ulimwengu huu wa smartphone uongo unajitenga mapema saana.
Elekeza nguvu kwenye kutafta pesa huku ukihakikisha kile kinachoendelea jamii inakijua.
 
Ni wazazi wenzetu lakini wengi bado vichwani wanautoto wa hali ya juu. Vumilia tu mkuu kuna siku atarudi kukutafuta. Kuna rafiki yangu imemtokea kisa kama hicho. Kazaa nae mtoto mmoja, mwanamke akakata mawasiliano eti anataka kuwa huru na maisha yake. Baada ya mwezi mmoja. Yule mwanamke akaanza kumtafuta tena jamaa kwamba anashida amsaidie. Sasa unajiuliza mwanamke kama huyu kichwa chake kipo sawa sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaumiza sana mkuu mara ghafla wanaibuka na kusema kama hutoi pesa za matumizi acha na uyu mtoto usimjue tena yani mambo ya hovyo kabisa mtu anakua kama nakubabaisha mara tuma pesa hapo hapo anasema kama hutaki acha aseeee ni kipengele.
 
Inaumiza sana mkuu mara ghafla wanaibuka na kusema kama hutoi pesa za matumizi acha na uyu mtoto usimjue tena yani mambo ya hovyo kabisa mtu anakua kama nakubabaisha mara tuma pesa hapo hapo anasema kama hutaki acha aseeee ni kipengele.
Nachoweza kukushauri mkuu, usitume chochote mpaka mzazi mwenzako atakapoona umuhimu wako. Kwa sasa wanakuchezea akili yako kwasababu wanakuona hauna msimamo. Kenge hasikii mpaka damu imtoke masikioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachoweza kukushauri mkuu, usitume chochote mpaka mzazi mwenzako atakapoona umuhimu wako. Kwa sasa wanakuchezea akili yako kwasababu wanakuona hauna msimamo. Kenge hasikii mpaka damu imtoke masikioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaio mkuu nikae kimya kwanza mpaka watakapo ona umuhimu na wanitafute wao wenyewe nitajaribu ivyo.
 
Si kila kitu cha kupeleka mahakamani.
Kuna mambo yakupasa unyamaze tuu ukiusoma mchezo.
Kukaa kimya kutakuepusha na mengi saana tena saanaa tuu.
Weka mikono 🙏muda wa ukweli ukifika hujidhihirisha.

Basi msilalamike watoto wakiitwa majina kutoka upande wa Mama zao ikiwa mimba zao zilikataliwa na Mama zao walitelekezwa
 
Baba kakataa mimba.
Baba kakataa kulea mtoto.

Sasa kwa nini mtoto aitwe kwa Jina lake?
Sio ishu ya chuki ili ni ishu ya Haki na wajibu

Mtoto anaweza kuitwa majina yako na ukaishi naye na ukamhudumia na akakuchukia licha ya kuwa Mama yake hayupo
Jina la baba ni kutokana na malezi au sababu za kibailojia??

Mbona kama unataka kupindisha sheria za ulimwengu ndgu??

Vipi mama akitelekeza wanae nae pia asitambiwe?? Kwenye cheti cha kuzaliwa aandikwe dada au mama wa baba yake??

Baba ni baba hata aweje ni baba yako, akukatae, akukubali, akukimbie itabaki hivyo milele, kamwe mjomba hawezi kua baba.

Mnaharibu maadili ndio maana vibinti vinazaa hovyo na kuleta vijukuu nyumbani. Huku kwa jeuri mkijiona mmemkomesha jamaa hamumpi mtoto jina la baba yake.
 
Single mama na watoto waliolelewa na single mama wamekuunga mkono.... je baba ambaye mtoto wake amepewa ubin wa mtu mwingine na anatakiwa amuhudumie mtoto hiyo ipo sawa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…