Mwanaume ambaye siwezi kuwa na mahusiano naye ni wa aina hii...

Mwanaume ambaye siwezi kuwa na mahusiano naye ni wa aina hii...

Mmh. Mleta uzi umesahau walishasema Wahenga "mchagua jembe si Mkulima".

Mie naona kikubwa kuridhiana na kupendana kwa dhati basi popote Penzi linaweza mea.
Weeeeh wahenga waongo hao.
 
Mmh. Hao ni wale vichwa maji kwa mwenye akili timamu hawezi kubadilika Mumy.

Daah,hakuna watu wanao badili tabia za watu kama marafiki. Hili linafahamika tangu miaka na mikaka,dahari kwa dahari. Mpaka ikasemwa kuhusiana na uchaguzi wa marafiki na athari zao. Ikasemwa hivi "Ukitembea na mfua vyuma,kama hautapata moja wapo katika mawili haya,yaani kama usiponuka harufu ya moshi basi cheche za moto hazita kukosa". Hii katika kuashiria tabia mbaya.

Na ikasemwa kuhusu uchaguzi wa marafiki wazuri,ikasemwa hivi "Ukitembea na muuza miski,kama usipovutiwa na harufu ya bidhaa yake ukainunua basi hata ile harufu kwa mbali utaipata"

Mapenzi au kupenda ni elimu ambayo wengi tumeitupilia mbali. Upendo ni zaidi ya kufata hisia na matakwa ya moyo.
 
1,Driver,hasa wa mabasi ya mikoani au malori ya mizigo ya masafa marefu kutoka nchi moja kwenda nyingine,,hapa kama una roho ya chuma ukubali kuwa mke wa 100 maana kila kituo,kila mkoa,kila mji ana mwanamke

2,driva tax na boda boda,hawa kama una moyo wa chuma ukubali kushare mapenzi na watoto wadogo,vibinti vya chipsi na secondary

3,Askari polisi ,hawa wanapenda wanawake wa kila aina,halafu hawana huruma,kumuumiza mwanamke ni jambo la kawaida.,halafu mkizenguana vitisho na hata mpenzi wako mpya anatishiwa

4,mafundi garage, hawa ni waongo,ukisha kuwa nae atakutangaza kwa kila mtu anayefanya kazi nae,na anapenda mwanamke awe anamfuata fuata kazini kwake kuomba matumizi

5,Wahudumu wa afya,madaktari na manesi nk,hawa hawana muda wa kuwaza mahusiano yenu,kila muda utamkuta yuko busy na vitu vidogo vidogo na akipumzika hataki bugudha yoyote,anataka apumzike mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera kwa uzoefu mkuu! Malizia upembuzi hata huku kwenye idara yetu naona umekua mama wa taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kukataa mtu mwenya hei na wewe na ukampenda mtu mwenye shari na wewe.

Hili hutokea sana. Mtazamo waki una dosari lukuki.
Mhhhhh! "Unaweza ukamchukia mtu kumbe ndiye mwenye heri na wewe na unaweza ukampenda mtu kumbe ndiye mwenye Shari na wewe"

Nimeipenda hii.
 
Na ukimpenda mtu wala hujari kazi ipi anafanya unachoangalia ni mapenzi bwana bado hajampata wa kumpenda

Hapa umeweka kauli ya jumla sana. Ila kupenda kwa mtindo huu ni ugonjwa.

Unajua mtu ukishajua kupenda maana nini,lazima utajua tofauti ya kupenda na kutamani. Na ukishajua hayo,utakuwa una amua mwenye upende au utamani.

Mathalani mimi kuna mabinti wa asili fulani,mlengo fulani,itikadi fulani,tabia fulani,kazi fulani siwezi kuwapenda na sijawahi kuwapenda. Sababu ninajua wapi pa kumwaga mbegu zangu.
 
Unajua kwa ujinga tulio nao katika suala la mapenzi yaani kupenda,kuna watu huwa wanafanya mambo ambayo hayawezekani.
 
1,Driver,hasa wa mabasi ya mikoani au malori ya mizigo ya masafa marefu kutoka nchi moja kwenda nyingine,,hapa kama una roho ya chuma ukubali kuwa mke wa 100 maana kila kituo,kila mkoa,kila mji ana mwanamke

2,driva tax na boda boda,hawa kama una moyo wa chuma ukubali kushare mapenzi na watoto wadogo,vibinti vya chipsi na secondary

3,Askari polisi ,hawa wanapenda wanawake wa kila aina,halafu hawana huruma,kumuumiza mwanamke ni jambo la kawaida.,halafu mkizenguana vitisho na hata mpenzi wako mpya anatishiwa

4,mafundi garage, hawa ni waongo,ukisha kuwa nae atakutangaza kwa kila mtu anayefanya kazi nae,na anapenda mwanamke awe anamfuata fuata kazini kwake kuomba matumizi

5,Wahudumu wa afya,madaktari na manesi nk,hawa hawana muda wa kuwaza mahusiano yenu,kila muda utamkuta yuko busy na vitu vidogo vidogo na akipumzika hataki bugudha yoyote,anataka apumzike mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulishapita nao wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom