Mwanaume Anatakiwa Awe Anajua Kupika au Kupika ni Suala la Wanawake Tu?

Mwanaume Anatakiwa Awe Anajua Kupika au Kupika ni Suala la Wanawake Tu?

New Designer

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2025
Posts
551
Reaction score
879

Habari wakuu,


Leo nataka tuzungumze kidogo kuhusu hili suala ambalo limekuwa kama mjadala wa kitaifa — je, mwanaume anatakiwa kujua kupika, au kupika ni kazi ya wanawake pekee?

Kuna hawa wanaume ambao hawajui kabisa kupika. Sijui kwa kweli wanaishije! Ila kwa uzoefu wangu, wengi wao ni wale watoto wa mama, au wale “wakina Junia” ambao hawajawahi kuishi ghetto peke yao. Wamezoea kila kitu kufanywa na mama au dada nyumbani.

Sasa cha ajabu, wakisikia mwanaume anajua kupika, wanashangaa sana — wengine hata wanamuita “amekosa kazi za kiume.” Lakini jamani, kupika ni kazi ya kike kweli? Hebu fikiria siku ukiwa peke yako, nani atakupikia? Au ukiwa na watoto wako na mama yao hayupo, mtakula nini? Utawaita majirani waje wapike?

Kuna msemo mmoja unasema, “Kama unajua kula, basi ujue pia kupika.”
Maana yake ni rahisi — huwezi tegemea tumbo lijazewe tu kila siku na mtu mwingine. Kuna siku utahitaji kujisaidia mwenyewe. Tuseme uko porini, au safari imekukuta mbali na nyumbani, njaa ikikukaba utawaua watoto kwa njaa ilhali unga upo ndani?

Kupika ni ujuzi wa maisha (life skill), si suala la jinsia.
Kama mwanaume unajua kuendesha gari, kuvaa suti, na kupanga bajeti, basi pia ni vizuri ujue kuandaa chakula chako. Hata wanawake wengi wanapenda mwanaume anayeweza kujihudumia — ni dalili ya kuwajibika na kujitambua.

Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu, kila mwanaume anatakiwa ajifunze kupika.
Sio kwa sababu anataka kuchukua nafasi ya mwanamke, bali kwa sababu ni ujuzi unaokuokoa kwenye maisha.
 
Wajinga ndiyo maana wakiwa kwenye ndoa wananyanyasika sana.....Mimi hakuna kazi ambayo siijui kuanzia kufua,kupika ,kupiga deki,kufagia uwanja ,kuchota maji,kulima majani etc kwahiyo mwanamke hawezi kususa halafu nikashindwa kufanya!!
Hawa hawajawai kuishi ghetto peke yao labda, ndio wale hata kulala peke yao wanaogopa Red black
 
Mimi najua sana kupika, kiasi kwamba mtu mwingine akipika naona kabisa kakosea. Yaani huwa nikienda hotelini naombaga kabisa jiko niwe najipikia.
 
Anatakiwa na nani ?

Nadhani hilo jibu inabidi awe nalo mtu husika kutokana an interest yake (by the way kama umesoma mpaka sekondari na umepitia chemistry nadhani utajua kuwasha jiko na ku-heat na kubadilisha from raw to cooked)

That said the top Chefs in the world they are Men....
 
Kila hotel ukienda utakuwa ukiomba jiko upike😂😁
 
Wakati nilipokuwa mdogo nafundishwa kupika, Mama alipenda kusema ni lazima ujue mahanjumati. Leo nimeshakua mkubwa nimeona faida.
 
Mke wangu alipojfungua nlikuwa ni mimi na yeye na mi ndiye nlimpeleka hospital nimebeba kila ktu, na nlimfata mi niye nikawa namkanda, nampkia, naosha vyombo, nafanya usafi mpk alipokaa sawa ninamaanisha kujua kupka kwa mwanaume n muhmu sn..
 
Si support hoja,
kazi yetu wanaume ni kutengeneza mifereji ya fedha tu.
kupika waachie kina mama unless we ni chief cooker.
Mwanaume inabidi uwe jeshi la mtu mmoja, sasa kama hata kujipikiabtu haujui inaonesha uko irresponsible
 
Back
Top Bottom