<div class="bbWrapper"></div>
- Tunachokijua
- Jambo hili lina ukweli. Huitwa Couvade Syndrome au Sympathetic Pregnancy.
Hali hii huwafanya wanaume wapate dalili za ujauzito kama vile kutapika, homa za asubuhi, kiungulia, kichefuchefu pamoja na kukosa usingizi.
Sababu za kutokea kwa hali hii huwa hazipo wazi sana lakini wasiwasi au furaha ya kuwa baba huhusishwa sana na kutokea kwake. Pia, ndoa au mahusiano yaliyopitia kwenye kipindi kirefu cha changamoto ya kupata mtoto hutoa nafasi kubwa ya kutokea kwa hali hii.
Mambo Muhimu Kuyafahamu
- Hutokea zaidi kwenye ujauzito wa kwanza
- Ni hali ya kawaida
- Dalili zake huwa kubwa kwenye miezi 3 ya mwanzo
- Hakuna dawa ya kutibu tatizo hili