KWELI Mwanaume anaweza kuonesha dalili za Ujauzito badala ya Mkewe

KWELI Mwanaume anaweza kuonesha dalili za Ujauzito badala ya Mkewe

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
MADAI
Mdau wa JamiiForums ametoa mkasa mmoja unaomhusisha mume wa rafiki yake wa kike aliyeanza kuonesha dalili za ujauzito kwenye ujauzito mchanga wa mkewe.

E47BFDD1-5E84-4AA0-8B07-7889ECEC23CD.jpeg

Mdau anaeleza kwamba shemeji yake huyu ilikuwa kila asubuhi anatapika njano, na homa za hapa na pale na kila alipoenda hospital Ugonjwa haukuonekana, ilifikia wakati mwanamme akawa hawezi kufanya shughuli zake kwa sababu ya kutapika sana.

Baada ya kupima ilikuja kugundulika kuwa mkewe alikuwa na ujauzito. Ikasemekena kwamba kuna nyakati fulani ujauzito anabeba mwanamke Ila mabadiliko na dalili za ujauzito anakuwa nazo mwanaume.

Jambo hili ni kweli au uzushi?
 
Tunachokijua
Jambo hili lina ukweli. Huitwa Couvade Syndrome au Sympathetic Pregnancy.

Hali hii huwafanya wanaume wapate dalili za ujauzito kama vile kutapika, homa za asubuhi, kiungulia, kichefuchefu pamoja na kukosa usingizi.

Sababu za kutokea kwa hali hii huwa hazipo wazi sana lakini wasiwasi au furaha ya kuwa baba huhusishwa sana na kutokea kwake. Pia, ndoa au mahusiano yaliyopitia kwenye kipindi kirefu cha changamoto ya kupata mtoto hutoa nafasi kubwa ya kutokea kwa hali hii.

Mambo Muhimu Kuyafahamu
  1. Hutokea zaidi kwenye ujauzito wa kwanza
  2. Ni hali ya kawaida
  3. Dalili zake huwa kubwa kwenye miezi 3 ya mwanzo
  4. Hakuna dawa ya kutibu tatizo hili
Kwa mujibu wa tafiti, hali hii huendelea kupungua kadri ujauzito unavyozidi kukua na huisha kabisa muda mchache baada ya kujifungua kwa mwanamke.
Na HCGH, homoni inayozalishwa na placenta wakati wa ujauzito inaonekana pia kwenye mkojo wa huyo mwanamume?
 
Iwapate tu manake wanaonaga kulea mimba ni kazi ndogo
 
Kisayansi hamna prove, ila kwenye mambo yetu mengine ndiyo nakubali kabisa.
 
Back
Top Bottom