Mwanaume anayemthamini/Mpenda Mchepuko kuliko Mke ni mshamba na anastahili kudharauliwa

Mwanaume anayemthamini/Mpenda Mchepuko kuliko Mke ni mshamba na anastahili kudharauliwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MWANAUME ANAYEMPENDA/MTHAMINI MCHEPUKO KULIKO MKE WAKE NI MSHAMBA NA ANASHTAHILI KUDHARAULIWA.

Anaandika, Robert Heriel.

Haijalishi Mke anamapungufu gani bado atabaki kuwa Mkeo na ndiye uliyemchagua Kwa hiyari yako.

Kama Mwanamke anakusumbua Kwa tabia mbofumbofu ni Akheri umfukuze/mpe talaka hiyo ni heshima zaidi kuliko Kujidharaulisha mbele ya jamii kwa kupenda michepuko kuliko Mkeo.

Moja ya Dalili ya mwanaume asiye na akili, aliyechanganyikiwa na ambaye hajitambui ni kuthamini mchepuko kuliko mkewe.

MWANAUME kamili hawezi kumkomoa mkewe Kwa kutomhudumia alafu ati ahudumie familia za nje ambazo hazimuhusu. Huyo ni punguani bila kujali nafasi yake, bila kujali umri wake, yaani ugombane na Mkeo ndio usitishe huduma Kwa hasira zako za kipumbavu. Ni bora umpe talaka utakuwa na hekima na Huko ndio kujiamini.

Talaka ni moja ya heshima ndani ya ndoa, kujiamini Kwa Mume au mke ikiwa hataki kujishushia heshima yake.

Mwanaume mshamba wa mapenzi, aliyejulia wanawake ukubwani ndio anaweza kupumbazwa na Michepuko ya nje, Kwa ufundi upi michepuko waliyonayo mpaka uisahau familia yako Kam sio ushamba wako Kwa wanawake.

Mwanamke yeyote ukimpa Uhuru katika mapenzi lazima umuone Fundi, lazima umuone anayajua mapenzi.

Sasa umemgeuza Mkeo Mtumwa, mfungwa wa mapenzi, hayupo huru alafu unamuona hajui mapenzi, wewe si kenge maji. Mapenzi na Uhuru vinapelekana, hakuna Uhuru hakuna mapenzi.

Embu fikiria ewe mwanaume mwenzangu, alafu utakuja kuniambia Kama wewe ni punguani au sivyo,
Mwanamke sio Mkeo. Mwanamke Hana mtoto hata mmoja wako, alafu unamhonga pesa au vitu ambavyo Mkeo hujawahi kumpa vitu hivyo, ukiulizwa alafu utumie akili utajiona nani kama sio lofa usiye na akili.

Bora hata vitu hivyo ungempa Mama yako ungeonekana unalipa walau Fadhila, na una akili.

Kwa wazoefu wa wanawake watakubaliana na Mimi kuwa, hawana jipya hivyo hakuna sababu ya mtu kuwa mzinifu, haya umeshindwa kujizuia uzinifu basi kuwa na akili hata kidogo.

Umechagua mke mwenyewe, kumaanisha ulimuona ni mzuri, kinachofuata ni kumtunza, kumpa mapenzi mtoto wa watu, zingatia mapenzi Kwa mwanamke yanahitaji mambo makuu Yafuatayo;

1. Attention
2. Muda wako
3. Uhuru wa mapenzi (mawasiliano)
4. Huduma

Zingatia, kama Mkeo ni Wale majianamke yasiyo jitambua, yanayohitaji kukupelekesha na kukupanda kichwani, usimuendekeze, usimpe nafasi.

Fukuza, mpe talaka

Asitumie kigezo cha ndoa kukuendesha Kama Gari bovu. Nilisema, hata Kama mmefunga ndoa ya Aina gani, hata kama ingefungwa wapi, Kama Mkeo Anakuletea za kuleta, Fukuza!
Mwanaume mzima unatishwa na upuuzi, mpaka unafikia hatua ati ya kuchepuka kisa Mkeo anakupimia, wewe ni Mpumbavu. Fukuza!

Uchepuke ukiwa unapenda kufanya hivyo ukijua ni Dhambi, lakini sio kisa kumkomoa Mkeo au Mkeo anakupimia.

Mwanamke usimuendekeze akijaribu kutingisha kibiriti, bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na muonekano wake.

Nimemaliza, povu Ruksa!

Sabato njema!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Muombe Mungu sana usijeingia majaribuni...kama sala ya Bwana isemayo.
Kuna wanawake wanajua kukamata kama super glue mkuu, ogopa sana

Maisha ni maamuzi Mkuu.
Ukiamua kukamatika unakamatika, lakini kuna umri ukifikia hakuna mwanamke atakayekuchanganya sema maamuzi tuu.

Ndio maana Vijana wanashauriwa wamalize ujana Kwa kujifunza mambo mengi, kuna umri ukifika unaona mambo mengi ya kawaida.
 
kuna vitu vingi vinapoteza mapato ya mtu binafsi.
unaweza ukajibana alaf unatoka tu na gari yako mara trafk paap laki imeenda,
mara bia,mara michango ya harusi,mara harambee.
oo umechaniwa mkeka,oo mashine za mchina,oo tumsaidie flani atoke hospitali.Mambo ni mengi,je,anayepteza pesa kwa hayo mengine wala haongi naye achangie wapi??
 
Uzi wa kishamba sana huu.

Mababa wa imani wote walikua na kazi za nje.

Ibrahim,

Isaka, Yakobo.

Hutapata sifa yeyote bila kua nao.
 
Kila mtu aishi anavyojua.wewe unaongelea mke wakati kuna wanaume wana wake,je unadhani hao wake walianzaje hadi kua wake kama hawakuanza kua michepuko.maisha ni yale unayoyaishi wewe.
 
Hii nayo ni Vita ya uchumi !! aise tutafika tuko hoi !!! haya Mambo ya ndoa haya ,ngoja niaichangie tu !!
 
Mkuu,

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili mume na mke wanaopendana, yaani mapenzi yakinoga , hukubaliana waishi pamoja.

Hili ni kundi la wengi ambao huumizwa kuzingatia na ule usumaku wa mapenzi kwa mwenzake.

Pili Kuna ndoa ambayo, mtu anajikuta lazima aoe ili kutimiza wajibu, au umri umeenda,

Au kama ni mwanamke mke anaolewa ili kulinda heshima, au kuishiwa mipango akiwa anatafuta pakuegemea,

Kundi hili ni rahisi mwanaume kumfukuza mkewe kirahisi tu kwakuwa hajamuoa kimapenzi Bali kiwajibu.

Mwanamke ni rahisi kudai talaka kwakuwa hana usumaku wa mapenzi ndani ya moyo wake kwako.

Mkuu mapenzi yasikie tu , huwezi kuyatabiri, kuyaelezea/kuchanganua yalikuwepo na yatakuwepo.

Said wa Mwanza alikuwa na hela si haba, alikuwa kijana ambaye akimtaka demu yeyote ingekuwa poa , lakini alipenda kiasi kisichoelezeka, hakuwekewa limbwata, la hasha.

Ni usumaku wa mapenzi ulimkamata akashindwa kujicontrol , yule dogo

Mapenzi shikamoo.
 
kuna vitu vingi vinapoteza mapato ya mtu binafsi.
unaweza ukajibana alaf unatoka tu na gari yako mara trafk paap laki imeenda,
mara bia,mara michango ya harusi,mara harambee.
oo umechaniwa mkeka,oo mashine za mchina,oo tumsaidie flani atoke hospitali.Mambo ni mengi,je,anayepteza pesa kwa hayo mengine wala haongi naye achangie wapi??

😃😃

Ndio umnunulie macho matatu mchepuko alafu Mkeo na Mama yako wanatumia simu za ajabu ajabu😊
 
Mkuu,

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili mume na mke wanaopendana, yaani mapenzi yakinoga , hukubaliana waishi pamoja.

Hili ni kundi la wengi ambao huumizwa kuzingatia na ule usumaku wa mapenzi kwa mwenzake.

Pili Kuna ndoa ambayo, mtu anajikuta lazima aoe ili kutimiza wajibu, au umri umeenda,

Au kama ni mwanamke mke anaolewa ili kulinda heshima, au kuishiwa mipango akiwa anatafuta pakuegemea,

Kundi hili ni rahisi mwanaume kumfukuza mkewe kirahisi tu kwakuwa hajamuoa kimapenzi Bali kiwajibu.

Mwanamke ni rahisi kudai talaka kwakuwa hana usumaku wa mapenzi ndani ya moyo wake kwako.

Mkuu mapenzi yasikie tu , huwezi kuyatabiri, kuyaelezea/kuchanganua yalikuwepo na yatakuwepo.

Said wa Mwanza alikuwa na hela si haba, alikuwa kijana ambaye akimtaka demu yeyote ingekuwa poa , lakini alipenda kiasi kisichoelezeka, hakuwekewa limbwata, la hasha.

Ni usumaku wa mapenzi ulimkamata akashindwa kujicontrol , yule dogo

Mapenzi shikamoo.

Umeongea maneno mazito sana mkuu
 
Back
Top Bottom