Mwanaume anayemthamini/Mpenda Mchepuko kuliko Mke ni mshamba na anastahili kudharauliwa

Mwanaume anayemthamini/Mpenda Mchepuko kuliko Mke ni mshamba na anastahili kudharauliwa

Whatever but ni mada ya kijinga ndio maana umekosa replies za kutosha.

Unafikiri kila mtu anaandika Kwa sababu ya replies au likes?

Ninaandika Kwa ajili ya mtu mmoja ambaye akisoma atabadilika na sio kila mtu.
Waliosoma naamini yupo mmoja niliyekusudia ambaye atakuwa amenielewa.

Kama ningekuwa naandika Kwa sababu ya Likes or replies ningeacha kuandika Mtandaoni miaka Saba iliyopita.

Soma, elewa, kisha toa maoni yako.

Karibu
 
Unafikiri kila mtu anaandika Kwa sababu ya replies au likes?

Ninaandika Kwa ajili ya mtu mmoja ambaye akisoma atabadilika na sio kila mtu.
Waliosoma naamini yupo mmoja niliyekusudia ambaye atakuwa amenielewa.

Kama ningekuwa naandika Kwa sababu ya Likes or replies ningeacha kuandika Mtandaoni miaka Saba iliyopita.

Soma, elewa, kisha toa maoni yako.

Karibu
Stupid
 
MWANAUME ANAYEMPENDA/MTHAMINI MCHEPUKO KULIKO MKE WAKE NI MSHAMBA NA ANASHTAHILI KUDHARAULIWA.

Anaandika, Robert Heriel.

Haijalishi Mke anamapungufu gani bado atabaki kuwa Mkeo na ndiye uliyemchagua Kwa hiyari yako.

Kama Mwanamke anakusumbua Kwa tabia mbofumbofu ni Akheri umfukuze/mpe talaka hiyo ni heshima zaidi kuliko Kujidharaulisha mbele ya jamii kwa kupenda michepuko kuliko Mkeo.

Moja ya Dalili ya mwanaume asiye na akili, aliyechanganyikiwa na ambaye hajitambui ni kuthamini mchepuko kuliko mkewe.

MWANAUME kamili hawezi kumkomoa mkewe Kwa kutomhudumia alafu ati ahudumie familia za nje ambazo hazimuhusu. Huyo ni punguani bila kujali nafasi yake, bila kujali umri wake, yaani ugombane na Mkeo ndio usitishe huduma Kwa hasira zako za kipumbavu. Ni bora umpe talaka utakuwa na hekima na Huko ndio kujiamini.

Talaka ni moja ya heshima ndani ya ndoa, kujiamini Kwa Mume au mke ikiwa hataki kujishushia heshima yake.

Mwanaume mshamba wa mapenzi, aliyejulia wanawake ukubwani ndio anaweza kupumbazwa na Michepuko ya nje, Kwa ufundi upi michepuko waliyonayo mpaka uisahau familia yako Kam sio ushamba wako Kwa wanawake.

Mwanamke yeyote ukimpa Uhuru katika mapenzi lazima umuone Fundi, lazima umuone anayajua mapenzi.

Sasa umemgeuza Mkeo Mtumwa, mfungwa wa mapenzi, hayupo huru alafu unamuona hajui mapenzi, wewe si kenge maji. Mapenzi na Uhuru vinapelekana, hakuna Uhuru hakuna mapenzi.

Embu fikiria ewe mwanaume mwenzangu, alafu utakuja kuniambia Kama wewe ni punguani au sivyo,
Mwanamke sio Mkeo. Mwanamke Hana mtoto hata mmoja wako, alafu unamhonga pesa au vitu ambavyo Mkeo hujawahi kumpa vitu hivyo, ukiulizwa alafu utumie akili utajiona nani kama sio lofa usiye na akili.

Bora hata vitu hivyo ungempa Mama yako ungeonekana unalipa walau Fadhila, na una akili.

Kwa wazoefu wa wanawake watakubaliana na Mimi kuwa, hawana jipya hivyo hakuna sababu ya mtu kuwa mzinifu, haya umeshindwa kujizuia uzinifu basi kuwa na akili hata kidogo.

Umechagua mke mwenyewe, kumaanisha ulimuona ni mzuri, kinachofuata ni kumtunza, kumpa mapenzi mtoto wa watu, zingatia mapenzi Kwa mwanamke yanahitaji mambo makuu Yafuatayo;

1. Attention
2. Muda wako
3. Uhuru wa mapenzi (mawasiliano)
4. Huduma

Zingatia, kama Mkeo ni Wale majianamke yasiyo jitambua, yanayohitaji kukupelekesha na kukupanda kichwani, usimuendekeze, usimpe nafasi.

Fukuza, mpe talaka

Asitumie kigezo cha ndoa kukuendesha Kama Gari bovu. Nilisema, hata Kama mmefunga ndoa ya Aina gani, hata kama ingefungwa wapi, Kama Mkeo Anakuletea za kuleta, Fukuza!
Mwanaume mzima unatishwa na upuuzi, mpaka unafikia hatua ati ya kuchepuka kisa Mkeo anakupimia, wewe ni Mpumbavu. Fukuza!

Uchepuke ukiwa unapenda kufanya hivyo ukijua ni Dhambi, lakini sio kisa kumkomoa Mkeo au Mkeo anakupimia.

Mwanamke usimuendekeze akijaribu kutingisha kibiriti, bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na muonekano wake.

Nimemaliza, povu Ruksa!

Sabato njema!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Asanteee
 
Huwa nafuatilia makala zako kwa umakini mkubwa. Uko vizuri mkuu. Sabato njema
 
😃😃

Ndio umnunulie macho matatu mchepuko alafu Mkeo na Mama yako wanatumia simu za ajabu ajabu😊
I nategemea mchepuko ameshawishi vipi hadi jamaa akafunguka.
Sasa ukute mke ni mdomo jalala, mchafu mchafu, moments zote na mumewe ni za makelele na kukera unadhani hata jicho moja atapata? Achilia macho matatu.
 
tutafute pesa za kutosha michepuko nayo ni binadamu inastahili matunzo tena wanashukrani hatari
 
Uzi wa kishamba sana huu.

Mababa wa imani wote walikua na kazi za nje.
Ibrahim,
Isaka, Yakobo.
Hutapata sifa yeyote bila kua nao.
Mleta mada kaogopa kugusia misahafu nadhani anajua picha halisi.
 
Mwanaume kuchepuka haimaanishi hampendi wala kumthamini mke wake.

Tutazulula weee lakini kwa wake zetu ndio kituo cha mwisho.

Sema wewe bado hayajakukuta .
Tumsamehe bure,
Mtoa mada hajaoa[emoji4]
 
Back
Top Bottom