Mnama
JF-Expert Member
- Oct 13, 2010
- 2,963
- 2,694
Jana nimecheka sana sana kwa sababu wadada walikimbiwa na kuachiwa bili baada ya kula na kunywa kama vile hawatakula tena.Walikuja na mwanaume aliyeonekana ana hela hawa wadada walikuwa watatu wanaonekana ni wanachuo wa chuo kimoja hapa tabora.
Wakaagiza mavinywaji machupa makubwa sijui yanaitwaje kila mtu moja moja yapo kama soda ya mirinda nyeusi.Jikoni wakaagiza kuku wawili na chipsy mayai kila mtu wakala zote kwa uroho hawajabakisha hata shingo waroho sana.
Huyo mkaka aliagiza tu maji makubwa basi.
Baada ya bili kupelekwa huyo mkaka akasema ngoja akatoe hela kwenye Atm kumbe akawa amekimbia moja kwa moja huku wadada walikuwa wanapiga stori wanagonga na mikono sijui walikuwa wanasema nini.Muda ulivyozid kwenda nahisi wakampigia simu haipatikani ikabidi waanze kuhaha wamekaaa hapo mpaka usiku saa 3 ndio kuna mdada mwingine akaja kulipa hela wakaondoka.Nikasema jaman pole yao tu wakome kudowea vya wanaume saivi wamekuwa wachoyo sana wabahili sana sana wanaume wamekuwa wachoyo .
Hamna sio wanaume wamekuwa wabahili ni kwamba wameerevuka hawataki ujinga..... unamuita mtu anakuja kafuatana na wenzie watatu unategemea nini .
Tena kuna wengine washenzi akifika ndio anawaita wenzie kwa simu unashangaa baada ya nusu umezungukwa meza imejaa watu hakya walahi utalipa mwenyewe....