Yimakatso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,063
- 12,171
Wanawake gani hao wanaotaka pesa ndiyo uwapate?View attachment 3396982View attachment 3396983
Mwanaume nisikilize!
Umasikini unauma zaidi ukiwa mwanaume. Familia inakutazama tofauti sana hata kama haikuambii ila we fahamu tu kuwa kuna vile wanawaza na kukutazama. Ukiwa huna pesa kuna namna fulani watu wanakunyima heshima au wanakukadiria heshima.
Ukiwa huna pesa hakuna anayejali unachosema haijalishi unasema point au jambo la maana kiasi gani. Na ukiendelea kutoa msisitizo ili point yako isikilizwe utaambiwa unapiga kelele au unaleta vurugu kwenye kikao.
Kwenye sherehe na misiba kama huna hela utawekwa kwenye kitengo cha kupasua kuni na kufunga maturubai bila kujali umri wako. Kama huna pesa watu hawaheshimu umri, watakukadiria heshima kulingana na kipato chako.
Tunaishi katika Dunia ambayo haina huruma kwa mwanaume asiye na pesa. Dunia ni sehemu katili kwa mwanaume masikini si Kanisani si hospitalini kama huna pesa wewe si lolote si chochote hata aina ya maombi utakayopewa na heshima utakayopewa ni tofauti sana.
Hata Kanisani wewe hata uwe na wanawake 6 na vimada 6 lakini una hela heshima yako italindwa, lakini kama huna pesa utatengwa. Hata Kanisa haliwapi kipaumbele wala heshima watu wasio na pesa.
Mwanaume amka kila siku ufanye kazi kwa bidii na kwa akili na maarifa — dunia ni katili sana kwa mwanaume maskini.
Hii inaweza kuwa inaumiza kuisikia lakini ndio ukweli mchungu.
Mbona mimi nazipiga free kabisa hadi inafikia mahali nazikwepa kwa kutoa visingizio vya uongo ili nipumzishe mwili.
Nipo very selective hapa mtaani nachagua mademu wabichi na wazuri ndiyo na deal nao.
Wewe kuna uwezekano mkubwa ukawa na sura isiyoeleweka kabisa ama ni mwenyeji wa kanda ile inayohonga sana wanawake kwa sababu ya inferiority complex mliyojijengea.