Mwanaume chukua somo kwenye kisa cha Talulah Riley na Elon Musk

Mwanaume chukua somo kwenye kisa cha Talulah Riley na Elon Musk

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
"Niliachana na Elon Musk baada ya yeye kuyumba sana kiuchumi lakini Kwa Sasa ninajutia kitendo changu cha kumuacha na sasa nataka kurudiana naye, sio kwa sababu ya Pesa zake nyingi Wala siyo kwa sababu amefanikiwa sana bali ninataka kurudiana nae kwa sababu ya Upendo wangu mkubwa kwake.
1737819473807.jpg


Kwa Sasa ninampenda sana tena kwa upendo wa dhati kabisa." Hayo ni maneno ya TALULAH RILEY, mke wa zamani wa Elon Musk. Musk Kwa Sasa ndiye Tajiri namba moja Duniani.

Akaongezea na kusema:
"Sikumuacha Elon Musk kwa sababu nilitaka kumuacha Bali ni kwa sababu alikuwa akipitia msongo mwingingi wa mawazo. Kwasababu Nilikuwa na wasiwasi kuwa atapata mshtuko wa moyo ndiyo maana nikamuacha. Iko hivi, Kipindi hicho Yeye na kampuni yake yote waliyumba kiuchumi, ingawa nilimuwacha lakini Nilikuwa nikimuomba Mungu amuweke hai mtu huyu na apate mafanikio.
images (90).jpeg


Mwaka huo hatimaye niliamua kumwacha Mwezi Desemba wakati aliposahau kuniletea zawadi ya Krismasi, hii ilikuwa krismasi mbaya sana kwangu, kwa sababu alisahau kuniletea zawadi ya Krismasi, Kipindi hicho tulikuwa tukiishi mji wa Kalorado na usiku huo kulikuwa na theluji nyingi kila mahali.
images (89).jpeg


Na tulipokuwa kitandani na nilipoomba zawadi yangu ya Krismasi, Elon alisema: 'Siyo kwamba sikupendi, ninakupenda sana, ila kwa Sasa ni kwamba ninapitia mengi magumu sana make wangu.'

Nikamjibu kuwa najua unanipenda..basi baada ya kusema vile aliamka usiku wa manane na kuondoka na kurudi baada ya masaa 2 na alikuwa ametoka nje kwenye theluji akiwa amevaa fulana yake na kaptula bila hata viatu pekupeku kwenye theluji na akaenda kunichumia maua.
images (91).jpeg


Na aliponipa maua yale akaniambia 'Nilitaka tu kukuonesha jinsi ninavyokupenda...' Lakini binafsi mimi sikupenda maua yale tena kwa sababu mimi sikuwa mtu fulani wa aina yake wa kuvumilia umasikini hivyo nikamwacha. Najuta kumuacha hivi sasa, bado nampenda na ninapenda turudiane na anioe tena." Talulah Riley.
images (90).jpeg


Kumbuka Mke huyu wa zamani wa elon Musk, Talulah Riley alimwacha wakati akiwa sio tajiri na akihitaji msaada wake zaidi lakini akamwacha.

Je ungekuwa nafasi ya Elon Musk ungemkubali tena mwanamke wa sampuli hii au ungeendelea na mambo zako?
 
Ni mwaka gani huo Elon Musk alikua siyo tajiri, Elon Musk katokea familia ya kitajiri tangu mdogo , yeye na kaka yake waligaiwa urithi mkubwa tu kaka yake ndo alitumia pesa vibaya ila yeye alikua na muendelezo mzuri wa hizo pesa na akamsaidia tena ndugu yake.

Au utajiri unaosemea ni hii ya kuwa tajiri namba 1?
 
Ni mwaka gani huo Elon Musk alikua siyo tajiri, Elon Musk katokea familia ya kitajiri tangu mdogo , yeye na kaka yake waligaiwa urithi mkubwa tu kaka yake ndo alitumia pesa vibaya ila yeye alikua na muendelezo mzuri wa hizo pesa na akamsaidia tena ndugu yake.

Au utajiri unaosemea ni hii ya kuwa tajiri namba 1?
Hesabu ya watu ni kuwa bi mdada anataka kumfanya Elon kuwa Jeff Bezos
 
musk hajawahi kuyumba kiuchumi, hii ni Stori yake ya uongo ambayo Baba yake anaipinga vikali. Labda kama alimdanganya huyo bibie. Wakati anaenda Marekani na kusoma huko kabla hajakuwa Bilionea alikuwa akipewa hela na baba yake toka Mgodi wa kimagendo walipokuwa wakichimba Emerald huko Zambia. Walikua na Emerald nyingi to the point wana Hela hadi kwenye masanduku hayafungi vizuri, so claim yoyote kwamba aliyumba kiuchumi ni ya kutunga.
 
Back
Top Bottom