Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Mwanaume halisi hatakiwi kuonewa huruma wala kujionea huruma Kwa sababu Mwanaume makini na mzuri ni yule aliyepitia magumu " the best men suffer". Haipo haja ya kumwambia mwanaume maneno laini kama una nia thabiti ya kumsaidia kuwa bora.
Ikumbukwe Mwanaume hujifunza zaidi kupitia ugumu na kukataliwa " Men always learn through negativity". Ipo Kila haja ya kulifanyia hii utafiti ila Sina mashaka na ukweli kuwa wanaume wengi wanaoonekana imara na bora leo nyuma ya pazia hawajapitia njia rahisi.
Wapo walioachwa yatima, waliotupwa magerezani na waliokataliwa kiasi ambacho hata leo wakikumbuka hawaamini. Wapo waliodhalilika na kudhalilishwa kuliko Mimi na wewe tunavyojiona leo lakini magumu hayo waliyoyapitia ni kama ngazi tu ya kupanda juu.
Vitabu vitukufu vinatuonesha mifano mingi sana ya wanaume waliokuwa imara sana na waliopitia madhila ya kutisha sana. Changamoto na matatizo ni darasa moja zuri na muhimu sana Kwa mwanaume.
Yupo msanii aliyewahi kuimba na katika wimbo wake alisema "wanaume tumeumbwa mateso". Hakika ni kama alifahamu njia ya kumnoa mwanaume ni mateso na kuhangaika haswaa.
Kujionea huruma ni kujichelewesha kufikia uimara na ubora unaotakiwa. Kanuni za ulimwengu zinamtambua mwanaume imara kuwa ni yule aliyejifinza kupitia magumu. Magumu yanapokuja ni Ili kujifunza na siyo kukata tamaa na kuacha kuendelea.
Ni ukweli tupo tunaopita katika hali tete sana lakini bado siyo sababu ya kujionea huruma na kuridhika na hali. Bado safari inaendelea licha ya uwepo wa vituo vingi njiani. Changamoto tunazopitia ni vituo vidogovidogo tu na siyo kituo kikuu ndiyo maana tunapaswa kuendelea mbele tu.