Mwanaume hauna wa kumlaumu zaidi yako: Jiangalie unachooneshwa mbaya wako ni wewe.

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Wanawake hawana tatizo lolote, tatizo ni sisi wanaume tutawalaumu bure ila mwisho wa yote tatizo ni sisi. Mwanamke anaishi kama kioo atakuonesha tu ujinga wako ulivyo utake usitake kwa kujua au kutojua. Amekuja kukusaidia wewe (Msaidizi) Kwa maana nyingine Mwanaume ndiye mwenye kazi haswaa. Mwanaume hakuumbwa Ili kuishi kama Mwanamke katika Dunia hii.

Ni jukumu la Mwanaume kukubali kubadilika ukishaoneshwa ujinga wako badala ya kulaumu, unalaimu nini sasa kama ukioneshshwa tatizo? Mi nadhani ukishaoneshwa tatizo suala la msingi ni kukubali kuwajibika wewe kama wewe siyo kutafuta wa kumlaumu.

Mwanamke kama ukikaa naye kizembe atakuonesha tu uzembe wako utake usitake, kuna watu tulishapitia hayo maisha tukajifunza ila Kwa kuumia sana. Unaweza ukalaumu ila mtu ila ukikaa peke yako kimya mahali tulivu kabisa na kujichunguza utabaini shida siyo wanawake.

Mwanamke ameumbwa kufanya mambo yake kwa hisia sana yaani karibu kila jambo alifanyalo anaangalia anajisikiaje kwanza. Anatawaliwa sana na hisia lakini Mwanaume anapaswa kufanya mambo yake bila kuangalia anajisikiaje. Hata kama hali ni ngumu vipi hata utamaduni unatufundisha kutojisikiliziasikilizia.

Maana ya hakuna anyempenda Mwanaume ni ukweli kuwa Mwanaume hapaswi kujionea huruma katika hali zote. Ni kiumbe aliyeumbwa Kwa mfano wa Mungu. Jiulize ni nani anamuonea Mungu huruma licha ya yeye kutupa kila kitu na bado tunamwomba na wengine tunakufuru kabisa.

Kuzaliwa Mwanaume ni sifa ya kipekee na bahati Kwa sababu Mwanaume ni alama ya uwezekano wa chochote kile. Mwanaume ni mtoaji, Mwanaume ni mlinzi n.k. Mwanaume hakuumbwa kupokea ila kutoa hata maumbile yetu ya uzazi yamekaa mkao wa kutoka ndani kuja nje tofauti na wenzetu ambao maumbile yao ni ya kupokea (yanaingia ndani).

Kwa mtazamo wangu Mwanaume kutoa ndiyo sifa yake ya asili na jukumu lake kuliko kupokea. Tusiogope tunapoona kila upande unatuhitaji kutoa Kwa sababu ndilo jukumu letu na siyo laana au hatia.
Inaendelea........
 
Hata ujauzito Mwanamke hupewa na kuutunza ndani mchakato wake ila baada ya miezi tisa hutuoneshea kilichokuwa kimetunzwa, tusipingane na asili Wanaume wenzangu.
 
🚮
 
Ni mtu mjinga tu anaendhani wanawake ni malaika. Yes kuna hizo scenario ambapo mwanaume anazingua na mwanamke ana respond as matukio yalivyo, but ni vibaya sana kudhani hawana shida, huwajui vizuri viumbe hawa
 
Ni mtu mjinga tu anaendhani wanawake ni malaika. Yes kuna hizo scenario ambapo mwanaume anazingua na mwanamke ana respond as matukio yalivyo, but ni vibaya sana kudhani hawana shida, huwajui vizuri viumbe hawa
Sijaandika lakini popote kuwa Wanawake wana kinga ya makosa au malaika ndugu ila nimesisitiza wanaume kuacha tu mchezo wa lawama " blame game" na kuwajibika tu.
 
Yaani kuwa mwanaume ni kufanya maamuzi bila kufikiri jinsi unavyohisi? Sasa huyo atakuwa mtu au Roboti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…