Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Wanaume wenzangu ebu tupeane ramani ya kudili na wanawake wenye drama,maana wengi wetu mnakufa kwa presha wakati familia zina wahitaji
Wanawake wana namna nyingi sana za kuwachanganya wanaume,ikiwemo kutaka kukufanya ujisikie wivu mnapokuwa public kwa kujiweka karibu na wanaume wengine,au wana kawaida ya kujiweka mbali na wewe kimapenzi kwa kujifanya hawajali kuhusu wewe
Ima katika mawasiliano,unaweza kumtext asijibu au asipokee simu yani hufanya makusudi tu kujua wewe ni mwanaume wa namna gani
Sasa usirogwe kulialia kwa hayo yote anayofanya,ukifanya hivyo unampa yeye mamlaka ya kukuendesha,mfano umetuma meseji hajajibu usianze kulialia na kulalamika mbona hujibu meseji zangu au hupokei simu zangu,hapo unaonyesha udhaifu mkubwa ambao ndio fimbo ya kukuchapa nayo
Au anajifanya kujiweka karibu na wanaume wengine makusudi uone wivu,usilalamike kwa nini unanifanyia hivi na vile
Unachotakiwa kufanya ni haya,mwambie huwa sipendi jinsi unavyojichanganya na wanaume wengine,sipendi mahusiano ya namna hii,kama unataka tuwe pamoja jirekebishe na kama huwezi sipo tayar kwa mahusiano ya namna hiyo
Hapo umemaliza sasa kama yeye anakupenda atakusikiliza na kama hakusikilizi ataamua mwenyewe kuachana na wewe,hapo wewe mwanaume haujapoteza kwasababu umeepuka kuwa na mtu ambaye haendani na viwango vyako,simpo iko hivyo yani,badala ya kulialia na kupoteza uanaume wako just be straight
Ima kwenye mawasiliano nayo hivyo hivyo kama hayupo kujenga mawasiliano imara,mpe option nataka mambo yaende hivi na si vile,tatizo wengi wetu tunaogopa kuyafanya haya kwa hofu ya kumpoteza mpenzi na matokeo yake,mwanamke anakuwa na power zaidi yako,zindukeni wanaume wenzangu,kuweni wanaume
Mwanamke vile vile anakawaida ya kukuingiza mtegoni kama yupo karibu na wewe halafu baadae anakaa hatua kadhaa mbali,yani ni drama tu,usiendeze ujinga,mwambie huwa napenda mambo ambayo yanaeleweka na sio michezo ya kuviziana,kama tunadhani huu uhusiano una afya tuwe serious
Ukifanikiwa katika mambo haya,utaokoa mambo mengi ikiwemo mda,kulinda hisia zako zisichezewe na mambo kama hayo,tambua kwamba hawa wanawake sometime wanafanya kwa makusudi au bila kujua,lkn nature ya mambo iko hivyo
Ni ǰuu yako mwanaume kuamua kuwa the living legend
Ni hayo tu!