Mwanaume huko Senegal avalia kama msichana kumfanyia mpenzi wake mtihani

Mwanaume huko Senegal avalia kama msichana kumfanyia mpenzi wake mtihani

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289

Mwanafunzi wa chuo kikuu huko Senegal yuko amejipata mashakani baada ya kuvalia kama mwanamke ili kumfanyia mpenzi wake mtihani wa somo la Kiingereza.

Picha za Khadim Mboup akiwa amevalia nguo za wanawake zimesambazwakatika mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari nchiniSenegal.

Mwanafunzi huyo wa miaka 22, ambaye alikamatwa mwishoni mwa wiki, alisema alikuwa akifanya hivyo kwa "kwa sababu ya mapenzi " kwa sababu mpenzi wake alikuwa na shida katika somo la Kiingereza, vyombo vya habari vya huko viliripoti.

Alifikishwa mbele ya korti Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa utambulisho na udanganyifu wa mitihani pamoja na mpenzi wake , ambaye alishtakiwa kuhusika katika uhalifu huo.
 
Nabaki Tanzania nitatuma na ya kutolea lakini kuvaa kama joti Fuc...k nooo.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Huyu ameenda extra miles sasa, badala ya kulipa ada(kumsomesha mchumba) ameamua kuingia kabisa front kufanya mitihani😂😂 na bado matokeo ya somo la kiingereza yakitoka amefaulu huenda angemuacha vile vile.😂hakika love is blind
 
Sijui kati ya hao wawili nani ana akili?aliyekuwa anafanya mtihani au aliyekuwa anafanyiwa mtihani
 
Huyu ameenda extra miles sasa, badala ya kulipa ada(kumsomesha mchumba) ameamua kuingia kabisa front kufanya mitihani😂😂 na bado matokeo ya somo la kiingereza yakitoka amefaulu huenda angemuacha vile vile.😂hakika love is blind
😅 😅 😅
 
Back
Top Bottom