Sina haja ya kujibu maswali ya kipumbavu. Cha muhimu jua kwenda sokoni ni kazi ya mwanamke.
Ukute wewe ni mwanamke umekosa bahati ya kuolewa sasa unaonea wivu wanawake wenzio
Mkuu haya ni maisha tu, na watu kama nyinyi ndo mnafanya maisha yaonekane magumu
Ishu ya mwanamke kwenda sokoni simzuii, akiamua anaenda kama sa hv nimeingia ndani nakuta kapika ndizi na aliniambia kabisa anaenda sokoni kununua ndizi,
Mimi nimechangia mada mkuu KURUDI NA MFUKO WA SOKONI
Kazi nafanya kariakoo, njia ya kurudi home ni lazima nipite kariakoo sokoni na hata nikiwa naenda ni lazima nipite kariakoo sokoni
Hivyo wewe unachopinga ni kusema, "Mwanaume utoke nyumbani uende sokoni kununua vitu". Wakati mimi nilichozungumzia ni kwamba mahitaji ya sokoni narudi nayo maana njia yangu ni kariakoo sokoni(hapa ndipo tunaposhindwa kuelewana)
Pia huwa naacha kodi ya meza kila siku japo kila kitu kipo ndani kwa hiyo mwanamke nimempa uhuru wa kuitumia pesa kwa mambo yake
Ndio mimi ni maskini lakini sijafika kukosa pesa ya kula, pia kula ndo kipaumbele changu, ninaposema kula sio kula ushibe hapana ni kula chakula bora
Maana umri wangu nahitaji kula vyakula vya kuimarisha Afya
Nakumbuka mwalimu wangu wa Biology aliwahi kuniambia, "Usipotumia pesa nyingi kwa chakula basi utatumia pesa nyingi kwa matibabu"
Nikutakie weekend njema mkuu