Chief,
Nakubaliana na wewe kabisa, tunajifunza kupambana na maisha kuanzia kwenye familia zetu
Kama watoto hawajapata msingi mzuri wa kujituma toka wakiwa makwao ukubwani itawapa shida sana
Hutukukulia vijijini lakini baba alinifundisha kujituma toka nikiwa mdogo,alikuwa ananiambia ipo siku moja nitakuwa na familia yangu
Tulibahatika kuwa na mashamba ya kiushikaji tulikuwa tunalima,kuvuna
Tulikuwa na bustani za mboga mboga,tulikuwa na ng'ombe kama wawili watatu ,nilikuwa nasafisha banda,nakamua maziwa,na kuna siku nilimsaidia kumzalisha ng'ombe kwa kumvuta ndama wakati anazaliwa
Mpaka leo nina alama ya kisu mkononi mwangu kidole cha kushoto wakati nakatakata majani ya magwatemala kwa ajili ya ng'ombe
Kwahiyo wazazi wafundisheni watoto namna ya kujituma na kufanya kazi,binti yako ajifunze kupika hata kama dada wa kazI yupo,siku moja moja afanye kazi za nyumbani,na kijana wako hivyo hivyo
Hapa chini angalia video ya watoto wa kishua baada ya kwenda likizo kwa bibi yao
View attachment 3514991