Kwa kiasi Fulani umesema kweli,ila wakati mwingine
ninyi wadada mnazengua kwa kujidhania mpo
matawi ya juu wakati muda mnafuatwa
mambo yakishawachachia ndo mnawakumbuka
wale mliowadharau,wakati huo wameishayapatia
maisha ndo mnaanza kujuta.
Mi nakumbuka nilimtokea mdada wakati
nataka kuoa,na ndo nimeanza kazi
nadhani aliona siko njema kiuchumi akanitema.
Mimi niliendelea kujiamini nikaona poa yote maisha./
Nilipokuja kumpata ambaye ni mke wangu kwa sasa
maisha yakakubali,nikapata kazi kampuni
nyingine,tukajenga na kupata usafiri,yule bidada
matawi ya juu akakaa akaona siku zinaenda
akajisogeza kwa jamaa wakafunga ndoa
maisha aliyonayo sasa tukikutana anaona aibu
uzuri huwa ananiamkia,lakini naamini moyoni
huwa anajuta.