Mwanaume kuvaa Kanga au Kitenge

Mwanaume kuvaa Kanga au Kitenge

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wadau Mimi naomba kuuliza kuna huu utamaduni naona unazidi kushamili sasa sijui hali ngumu za maisha. Kuna kasumba siku hizi imekuwa kama Fashion wanaume kuvaa Kanga au Kitenge hasa asubuhi nje wakati kupiga mswaki au ata mida mingine tu ya kawaida ukienda kumtembelea mtu badala taulo au msuli.

Huu utamaduni wa wapi?
 
Kanga na vitenge ni mavazi ya wanawake, kwahiyo mwanaume akivaa vazi hilo, anakuwa amejifananisha na wanawake, na hili jambo baya kabisa.

Misuli ndiyo mavazi yetu, tuvae misuli ama kanga na vitenge ni mavazi ya wanawake.

Ahsante.
 
Kanga na vitenge ni mavazi ya wanawake, kwahiyo mwanaume akivaa vazi hilo, anakuwa amejifananisha na wanawake, na hili jambo baya kabisa.

Misuli ndiyo mavazi yetu, tuvae misuli ama kanga na vitenge ni mavazi ya wanawake.

Ahsante.
Haahah hii nooma sana
mimi hata barakoa ya kitenge akivaa man najisikia hovyo
 
Huu ni utamaduni wa kiswahili wa zamani Sana, kwa mwanamke Kiswahili hasa wa ki Zanzibar. Wanahisi Mwanamme kuvaa bukta,suruali kipande wakati yuko chumbani na mkewe ni kumvunjia heshima mke wake..
 
Nguo ni nguo tu, sisi kwetu bara hatuna hayo mamisuli, unyamwezini tunavaa tu hizo kanga na vitenge. Hamna shida hata lubega wa kitenge au kanga tunapiga tu.

Mijini kuvaa kanga au kitenge asubuhi ukiamka na kutoka chumbani kwangu ni vazi tu jepesi nimevaa, mke wangu ameniandalia kanga moja ndo huwa navaa.

Nisipoiona huwa naibua yoyote ile. Kwake ni furaha tele. Nikiondoka inafuliwa na kutunzwa.
 
Kaka na vitenge ni mavazi ya wanawake, kwahiyo mwanaume akivaa vazi hilo, anakuwa amejifananisha na wanawake, na hili jambo baya kabisa.

Misuli ndiyo mavazi yetu, tuvae misuli ama kanga na vitenge ni mavazi ya wanawake.

Ahsante.
Vipi suruwali zile hasa jeans mbona wanawake wanavaa Sana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kwetu Mabibo wanaume wanavaa khanga misibani na jioni wakienda kucheza bao. Naona huko mbeleni wataanza kuvaa sidiria na bikini pia.
 
Back
Top Bottom