Mwanaume kuvaa Kanga au Kitenge

Mwanaume kuvaa Kanga au Kitenge

Nguo ni nguo tu, ss kwetu bara hatuna hayo mamisuli, unyamwezini tunavaa tu hizo kanga na vitenge. Hamna shida hata lubega wa kitenge au kanga tunapiga tu.

Mijini kuvaa kanga au kitenge asubuhi ukiamka na kutoka chumbani kwangu ni vazi tu jepesi nimevaa, mke wangu ameniandalia kanga moja ndo huwa navaa.

Nisipoiona huwa naibua yoyote ile. Kwake ni furaha tele. Nikiondoka inafuliwa na kutunzwa.
Aisee!! una miaka mingapi kwenye ndoa?
 
Limbwata hilo bwashee.

KENZY njoo uone [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mambo ya Pwani yananichanganya,
Vitu fulani wanavyofanya.

Dume zima shanga kiunoni, nini hizo khanga.

Solo Thang.
 
Tabia za watu wa mwambao.....
kanga, kitenge msuli vipo karibu karibu tofauti ni material tu
 
Tuache ushamba, kujifunga kitenge au kanga kiunoni, wakati wa kwenda kuoga wala siyo ushamba. Maeneo ya pwani tunakabiliwa na joto, kipindi kirefu cha msimu kuliko baridi, hivyo tunajifunika nguo nyepesi kanga au kitenge. Na wanaojifunga hivyo wengi ni wanaume, walio owa nasisitiza walioa, na wengi wanaishi maisha ya chini kiuchumi.

Huko kwenu kama mnatoka na shuka au blanketi kwenda kuoga, hatuwapangii, tokeni tu. Ila vazi la kitenge si ndo tulichagua Tanzania, kama vazi la Taifa, kuvaa shati la kitenge kwa anaelewa siyo tatizo wala barakoa ya kitenge, na kwa mwanamme kitenge kujifunga kiunoni. Maana hakuna mwanamke anaejifunga kitenge kiunoni, hapo ndipo tofauti inapo onekana.
 
Wakivaa ama wasipovaa kuna tofauti yoyote?

Unadhani jua litaacha kuzunguka kwenye muhimili wake kwa kuwa tu wewe mtu mmoja usiyejulikana hata jina umevaa Kanga??

Unataka tujadili nini haswa? Tukukataze usivae Kanga ama?
 
Back
Top Bottom