Mwanaume limbukeni

xixi

Senior Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
184
Reaction score
350
Habari..

Nimetamani kushare kuhusu mwanaume limbukeni.

Yule ambae anahisi akikupa ela ndo kamaliza kukupenda na kukujali. Ambae mali yake kila siku inaliwa na vijana wa mtaani, wachora kucha, bodaboda, waha wakopesha vyombo nk.

Halafu unakuta kuna mwamba huku ndani anaijua hii, ila anaona akiawasanua mkisanuka wake zenu atawakosa.

Acha ulimbukeni, upweke hauliwazwi kwa pesa, jiongeze ili uepukane na vilio vya hapa na pale pindi ukisalitiwa.
Asanteni
 
Tatizo la wanawake wa Siku hizi wakiona mwanaume kajitoa kuwapa Pesa na upendo wanamuona Limbukeni na Mjinga..

Ngoja nikupe facts..
MWanaume hatoi pesa hovyohovyo ila kwa sehemu anayoithamini nakuipenda..
Ipo siku atashtuka kuwa hapendwi na hataweza kukupa tena Hiyo pesa unayomuonea nayo ulimbukeni..

Hatutaki kuona Uzi tena na mabandiko yanayosema wanaume ni wabahili na hawajali wapenzi wao..

Wanawake hamjui Mnalotaka hamjui nini hasa mnataka mpewe na hasa nyinyi wanetu wa 2k..

Yaani mnahisi Mnaijua Dunia kuliko sisi Baba zenu?
 
Naona una dalili za kutafuta justification za usaliti kwa mume wako.
Once msaliti always msaliti usitafute visingizio vya kuhalalisha kugawa kwa kila msela anayepita mbele yako.
 
Asante mzee wangu kwa hii nondo.
 

Nimekumbusha tu kwa kuwa baba zetu mnatumia pesa kama silaha ya kuangamiza mapenzi ya dhati na kujali, nafasi zenu mnazijaza na pesa sisi ndio tuwape mapenzi tuwajali kumbe pesa sio chochote kwenye uhalisia wa mapenzi ya dhati.
 
Itabidi tumsubiri yule mwamba anaetupia ndoano kwa samaki bila kuweka dau lolote halafu samaki wanajaa wanapigana wanauana wasimkose mwamba..
Mimi ni samaki tu.
Ukipandisha mada ujue kuidefend kwa hoja zinazoibuka, hujanijibu mkuu.
 
Kwa utamu gan?
 
Nimekumbusha tu kwa kuwa baba zetu mnatumia pesa kama silaha ya kuangamiza mapenzi ya dhati na kujali, nafasi zenu mnazijaza na pesa sisi ndio tuwape mapenzi tuwajali kumbe pesa sio chochote kwenye uhalisia wa mapenzi ya dhati.
Mkuu hayo ya pesa ni nyie, kwahiyo hamzitaki pesa tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…