Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa mfafanuo mzuri...Wakulungwa huyu binti ana hoja nzito! Mahusiano haşa ya mapenzi si kitu rahisi kama wengi tunavyodhani. Kila upande katika mapenzi una vipaumbele vyake. Ni kosa kwetu wanaume kudhani hela ndicho kipaumbele cha kila mwananke. Kuna wengine kweli ni kipaumbele lakini wengine hela ni kichocheo cha mapenzi ingawa ni muhimu katika maisha ya mwanadamu ya kila siku.
Hii imenikumbusha jinsi ndoa ya Rafiki yangu ilivyoyeyuka baada ya miaka 25. Yeye kwa vile alizaliwa katika familia maskini ila kichwani si haba, alipokwenda kuchukua PhD ikabidi aambatane na familia yake. Pamoja na kusoma alifanikiwa kupata kazi chuoni za kupublish, hivyo alikuwa busy ofisini hadi wakati mwingine kurudi kwake ilikuwa ni saa 9 usiku.
Ni mengi ila familia ilipoteana kabisa maana
Familia ilijiona ameitupa ingawa alikuwa anatafuta pesa na kuitunza kama head of household.
Nazidi kukazia kuwa xixi ana hoja, hebu wanaume wa shoka hapa JF muitafakari kwa makini hasa wakati huu sisi tunaofunga!
Umenijibu kistaarabu hadi najiona fala, samahani kwa kutumia lugha ya kero.huu ni mfano ambao umebase kwa watu walio karibu na wanawake kwa namna moja au mbili
Ikishafikia hatua tamu ya Mume wako unawagawia hadi Bodaboda,Wachora Kucha,Wakopesha Vyombo basi hapo ujue huna mke...Habari..
Nimetamani kushare kuhusu mwanaume limbukeni.
Yule ambae anahisi akikupa ela ndo kamaliza kukupenda na kukujali. Ambae mali yake kila siku inaliwa na vijana wa mtaani, wachora kucha, bodaboda, waha wakopesha vyombo nk.
Halafu unakuta kuna mwamba huku ndani anaijua hii, ila anaona akiawasanua mkisanuka wake zenu atawakosa.
Acha ulimbukeni, upweke hauliwazwi kwa pesa, jiongeze ili uepukane na vilio vya hapa na pale pindi ukisalitiwa.
Asanteni