Wakulungwa huyu binti ana hoja nzito! Mahusiano haşa ya mapenzi si kitu rahisi kama wengi tunavyodhani. Kila upande katika mapenzi una vipaumbele vyake. Ni kosa kwetu wanaume kudhani hela ndicho kipaumbele cha kila mwananke. Kuna wengine kweli ni kipaumbele lakini wengine hela ni kichocheo cha mapenzi ingawa ni muhimu katika maisha ya mwanadamu ya kila siku.
Hii imenikumbusha jinsi ndoa ya Rafiki yangu ilivyoyeyuka baada ya miaka 25. Yeye kwa vile alizaliwa katika familia maskini ila kichwani si haba, alipokwenda kuchukua PhD ikabidi aambatane na familia yake. Pamoja na kusoma alifanikiwa kupata kazi chuoni za kupublish, hivyo alikuwa busy ofisini hadi wakati mwingine kurudi kwake ilikuwa ni saa 9 usiku.
Ni mengi ila familia ilipoteana kabisa maana
Familia ilijiona ameitupa ingawa alikuwa anatafuta pesa na kuitunza kama head of household.
Nazidi kukazia kuwa
xixi ana hoja, hebu wanaume wa shoka hapa JF muitafakari kwa makini hasa wakati huu sisi tunaofunga!