Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MWANAUME MPUMBAVU NDIO HUMPIGIA MKEWE MAGOTI;. JIONYESHE KUWA MWANAMUME
Anaandika, Robert Heriel
Shahidi
Mwanamke pekee ambaye mwanaume anaweza kumpigia magoti ni Mama yake.
Na hapa nazungumzia mwanaume sio mvulana. Nazungumzia mwanaume mwenye umri kuanzia miaka 20.
Mwanaume atapiga magoti Kwa mamaye Kwa Sababu kuu mbili;
Mosi, kutaka baraka za Mama.
Pili, kuomba radhi/msamaha ikiwa ametenda kosa KUBWA linalostahili laana.
Mwanaume ndiye mungu wa Dunia Hilo halina ubishi. Kama vile Mungu Mkuu asivyoweza kumuangukia, kumpigia magoti mwanadamu ndivyo ilivyo hata Kwa mwanaume hatakiwa kumuangukia na kumsujudia Mwanamke.
Ukitaka mwanamke akuone hamnazo, akudharau, akuone popoma, akushushe na kukuona hujielewi basi mpigie magoti.
Magoti yanamaanisha, unyenyekevu, kujishusha, kujisalimisha, kuhitaji msaada, kuhitaji wokovu, kushindwa nguvu. Hayo ndio magoti.
Elewa kuwa wanawake wanapenda mwanaume halisi, mwanaume mwenye nguvu, sio nguvu za mwili tuu Bali nguvu za kihisia, kimtazamo, kiakili, kiroho na nguvu za kiuchumi.
Hakuna mwanaume mwenye nguvu alafu akajisalimisha au kumpigia mkewe magoti, haijawahi kutokea na kamwe haitokuja kutokea.
Wanawake tuu wenyewe Kwa wenyewe Siakolojia Yao hawawezi kupigiana magoti kwani wanaona huko ni kujidharau.
Usijefikiri ukimpigia Mkeo au mwanamke magoti ndio ataona unampenda. Kuna namna nyingi za kuonyesha upendo wako Kwa mwanamke akakuelewa na akafurahi kuliko Kupiga magoti. Mwanamke ukimpigia magoti Jambo atashtuka na mshtuko wake utauona machoni mwake. Atakushangaa Sana. Alafu hataamini kuwa wewe ni Mpumbavu Kwa kiwango hicho.
Zingatia hata mwanamke mwenyewe kukupigia magoti wewe mwanaume ni mpaka awe anakupenda mno,
Mwanamke haoni shida kupiga magoti Kwa mtu anayekupenda tena kwake atajihisi fahari na hiyo itamaanisha yupo chini yako, anakuaminia, wewe ndiye kiongozi na Jemadari wake, amejisalimisha kwako umfanyie utakavyo.
Mwanamke kama hakupendi hawezi kujipigisha magoti hapo na kujishusha, hawezi na hatokuja aweze.
Hata hivyo Umasikini unaweza kumfanya mwanamke afanye maigizo ya kukupigia magoti.
Hata ufanye kosa gani Kwa Mkeo, hakuna kupiga magoti, Kama hataki kukusamehe achana naye, kila mmoja aendelee na hamsini zake.
Siku utakayopiga magoti ndio siku ambayo sio tuu utajiaibisha mwenyewe Bali hata Mama na Baba yako wakikuona wataona walizaa cherema, Popoma, lofa. Yaani utawaabisha mno.
Ukiwa mwanaume lazima uishi Kama Mwanaume. Ujionyeshe kama Mwanaume. Useme na utembee kama Mwanaume. Ufikiri na kuwaza kama Mwanaume. Sio uwe na mambo ambayo hata Wanawake wenyewe hawana. Huo ni ushoga. Yaani wanawake wenyewe wakikuangalia wanakushangaa kuwa wewe ni mwanaume au kitu gani.
Nakuhakikishia, mwanamke unaweza kumuoa akiwa mwaminifu kabisa lakini matendo yako ya ajabuajabu yanaweza kumfanya atafute mwanaume ambaye ni mwanaume halisi.
Hata kama unampa pesa, unamtunza mkeo, hayo yote Mkeo anaweza kuyapata mwenyewe.
Mwanamke anachotafuta Kwa mwanaume ni kile ambacho yeye Hana, anatafuta Uanaume.
Msikilize Daudi anapompa mausia mwanaye Suleiman; zingatia iliyokolezwa.
1 Wafalme 2:1
Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema
1 Wafalme 2:2
Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume;
Huo ndio usia Bora ambao Baba au mama anaweza kumuusia kijana wake.
Jionyeshe kuwa Mwanaume.
Sio unaleta mambo ya ajabuajabu
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam