SI KWELI Mwanaume mwenye vipele vidogo kwenye kichwa cha uume hawezi kupata UKIMWI na magonjwa ya zinaa

SI KWELI Mwanaume mwenye vipele vidogo kwenye kichwa cha uume hawezi kupata UKIMWI na magonjwa ya zinaa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Penile.jpg

Nimeona huko walimwengu wakijadili kuhusu vile vipele vinavyozunguka kichwa cha uume, sasa baadhi wanadai kuwa mwanaume mwenye hivyo vipele ana asilimia ndogo sana ya kuambukizwa UKIMWI hasa akiwa na damu group O-, lakini pia mwanaume mwenye navyo hawezi kupata magonjwa ya zinaa.

Haya mambo yanachanganya, tusije jikuta tunalombana bila tahadhari tukapata majanga.

Naamini humu tutapata uhalisia wa hili.
 
Tunachokijua
Vipele vidogo vitokeavyo kwenye kichwa cha uume kitaalamu hujulikana kama Pearly penile papules ambavyo mara nyingi hutokea baada ya mwanaume kubalehe. Vipele hivi hutokea kwa kuzunguka kichwa cha uume vikiwa vimepangana kwa kufuatana kuzunguka kichwa cha uume. Vipele hivi sio vya kuambukiza na wala huwezi kumuambukiza mtu.

Magonjwa ya zinaa (ngono) huambukizwa kwa njia ya ngono mfano Kaswende na Kisonono, wakati mwingine huweza kuambukizwa kwa njia isiyo ya kufanya ngono moja kwa moja mathalani mama anaweza kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua. Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) takribani watu milioni moja kila siku wanapata magonjwa ya zinaa yanayotibika huku wengi wakiwa kati ya miaka 15-49, na wengi wao wakiwa hawaoneshi dalili.

Tovuti ya MedicalNewsToday wanabainisha kuwa bado haijabainika haswa vipele hivi (Pearly penile papules) vinasababishwa na nini, na badala yake inaaminika kuwa vinatokea katika hali ya kawaida tu. Haviambukizwi kwa njia ya ngono, na wala havisababishwi na viambukizi (infections) au magonjwa, havina hatari kwa mtu mwenye navyo. Huwezi kujikinga na vipele hivi na wala havina matibabu maalum ingawa kuna baadhi ya njia ya kuvitoa zinazotolewa na wataalamu wa afya ikiwa mtu hatokuwa na amani kuwa navyo.

Makala ya Health.com inaeleza kuwa vipele hivi vya (PPP) ni hali ya kawaida ya utofauti wa ngozi, na havina madhara ama hatari yoyote, pia kuwa navyo haina maana kuwa vinakuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa mengine.

Hakuna uthibitisho unaoonesha kuwa mtu mwenye vipele hivyo hayupo katika hatari ya kupata UKIMWI ama magonjwa ya zinaa. WebMd wameandika kuwa kama una vipele hivi na umekuwa ukishiriki ngono ukijihisi una magonjwa ya ngono nenda ukamuone daktari na ukamueleze unavyojihisi.

Tovuti ya NIH inaeleza kuwa ni vyema kuchukua hatua mbalimbali ili kuweza kujilinda na UKIMWI ikiwemo kutoshiriki ngono zembe, kutokuchangia vitu vyenye ncha kali pia unaweza kutumia kondomu.

Nimeona huko walimwengu wakijadili kuhusu vile vipele vinavyozunguka kichwa cha uume, sasa baadhi wanadai kuwa mwanaume mwenye hivyo vipele ana asilimia ndogo sana ya kuambukizwa UKIMWI hasa akiwa na damu group O-, lakini pia mwanaume mwenye navyo hawezi kupata magonjwa ya zinaa.

Haya mambo yanachanganya, tusije jikuta tunalombana bila tahadhari tukapata majanga.

Naamini humu tutapata uhalisia wa hili.
HIo ishu umeisikia wap? Maana kwenye Ukimwi ni virus na magonjwa ya zinaa ni Bacteria habagui kabisa group la damu au hivyo vipele ni kupenya tu kwenye mrija wa haja ndogo na kuingia kwenye Damu.

#JE WAJUA, KATI YA SINDANO YENYE MAUMIVU DUNIANI NI YA GONO
 
Nimeona huko walimwengu wakijadili kuhusu vile vipele vinavyozunguka kichwa cha uume, sasa baadhi wanadai kuwa mwanaume mwenye hivyo vipele ana asilimia ndogo sana ya kuambukizwa UKIMWI hasa akiwa na damu group O-, lakini pia mwanaume mwenye navyo hawezi kupata magonjwa ya zinaa.

Haya mambo yanachanganya, tusije jikuta tunalombana bila tahadhari tukapata majanga.

Naamini humu tutapata uhalisia wa hili.
Wazee hii ni kama inamake sense binafsi mimi hivo vipele ninavyo na ninavyo toka kitambo sana na sijuag vilikuja kwanini.

Cha kushangaza kama umefatilia nyuzi zangu nilishawahi kuwa na Dem ana sijuwi ni uti sugu ile au niliitaje lile gonjwa lakin kwangu mm lilidunda.

Kwenye ukimwi sijuwi na sitak kufanya research ya vitendo
 
Kuna ukweli hapa, Kwa umri huu wa 42yrs sijawahi Hata kuumwa mkojo mchafu Wala gono Wala muwasho kichwani, na nazichakata kwelikweli😊
dogo kazana.,binafsi nilikua kama wewe sasa niko umri wa uzee na bado napiga huwa najiuliza vijana wako wapi hadi wazee tunawasaidia jukumu lao kwa kweli nimefurahi kusikia vijana kumbe mpo japo kwa uchache kwenye ndani ya sekta
 
Sijui kama hii tafiti ni kweli au uongo ila nipo hivyo na kiukweli sijawahi kupata gonjwa lolote la ngono,

Kuna kipindi kama Miaka miwili imepita nilishiriki Ngono bila kinga na binti mmoja hivi baada ya siku mbili nikaanza kukojoa Uji uji mweupe kama usaha ila baada ya siku mbili kupita ile hali ikaisha hata bila kunywa dawa yoyote.
 
Kuna mtu alipata tatizo la zinaa kwa mda mfupi kisha likapotea na akawa sawa kabisa, siku moja akaamua tu aende hospitali kufanya check up, daktari akamwambia mshukuru MUNGU mno maana ulikuwa unaenda kupoteza uzazi kwa mashambulizi ya ndani kwa ndani. Nasikia kuna gonjwa la zinaa linafanyaga maujinga ujinga halafu linapotea kama halipo vile ila lipo ndani kwa ndani, likirudi tena nje ukaanza kukojoa usaa sijui damu ndo lishamaliza kazi unakuwa huna uzazi.
 
Kwa mwanaume uzaz unaharibikaje mkuu ?? Kwa mwanamke nnavyojua ugonjwa hushambulia mirija ya fallopio na kuizba mpaka inashndwa kupitisha manii!! Nifafanulie Kwa mwanaume how uzaz unaweza haribiwa ??
 
Kwa mwanaume uzaz unaharibikaje mkuu ?? Kwa mwanamke nnavyojua ugonjwa hushambulia mirija ya fallopio na kuizba mpaka inashndwa kupitisha manii!! Nifafanulie Kwa mwanaume how uzaz unaweza haribiwa ??
Sasa boss uume usiposimama utazalishaje? Au utauingiza kama utambi?

Magonjwa kama Syphilis inaweza ikadisupt nerve signals ambazo zinahusika na uume kusimama, Chlamydia, Gonorrhea kama zisipotibiwa zinaweza leta tatizo la kutokusimama uume.
 
Back
Top Bottom