Mwanaume mwenye wake 15 asema Wanaume wenye Mke Mmoja wana Akili Ndogo Sana: "Wanaweza Kuongelea jambo moja kwa saa 3”

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Mwanamume mmoja ambaye ni mume wa wanawake wengi amewachamba wanaume ambao wameoa mke mmoja tu.

Kaluhana mwenye umri wa miaka 63 anasema wanaume wenye mke mmoja wana akili ndogo sana na hawezi kuelewana nao kwa sasa Kaluhana ana wanawake 15 nchini Kenya na Uganda na anasisitiza kuwa hatachoka kuongeza wanawake.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, David Zakayo Kaluhana anasema kuwa wanaume wenye mke mmoja wana akili ndogo sana na kamwe hawezi kuelewana nao.
Kaluhana mwenye umri wa miaka 63 anatoka eneo la Malava kaunti ya Kakamega na amejaaliwa kuwa na wake 15.

Kulingana naye, wanaume wenye mke mmoja wana upungufu wa akili na fikra kwani akili zao zinazunguka tu kwa suala moja kwa muda mrefu tofauti na wanaume wenye wake wengi.

Kaluhana ambaye amejaliwa watoto 107 amesema kuwa alikuwa mwerevu sana kuishi na mke mmoja na hapo ndipo akapata msukumo wa kutafuta wake wengi. Mwanamme huyo ameeleza kuwa anahakikisha kuwa anawapa wake wake wote chakula na kumjali kila mmoja Kaluhana amefichua kuwa yuko na wake hadi taifa jirani la Uganda na kuwa mpango wake huo wa kuwa na wake wengi haukomi hivi karibuni.

"Zaidi wanakuja. Hii sio mwisho. Siwezi kusema lini nitakoma lakini kama wanapewa mahitaji yao watakuwa sawa," alisema Kaluhana.

Video:
 
Mfalme Suleiman alikuwa na Ke 700 na Vimwana 300, aendelee kukaza fuvu ilihali chini ya jua hakuna jipya zaidi ya kuufukuza upepo tu [emoji847]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Nikola Teslas na Isaac Newton hawakuwai kuoa na leo wapo kwenye historia ya watu wenye akili zaidi waliowahi kuishi hapa duniani.
Hahaha..!! Nadhani jamaa ana vigezo vyake vya "akili".
 
Naomba kufahamu yeye mwenye wake wengi jambo moja analiongea kwa muda gani?
 
Ni kweli kabisa.

Hata migogoro mingi ya ndoa ni kwa wenye mke mmoja.

Hata nje ya ndoa; ukiwa na girlfriend ni rahisi sana kuteswa na mapenzi tofauti na mwenye girlfriends.

Ana hoja, asikilizwe.
Asitupiwe mawe!!
 
Back
Top Bottom