Mwanaume, umewahi kufika mahali ukamwaga chozi kwa sababu ya ugumu wa maisha ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Chozi la mwanaume kwenye mapambano ya maisha ni kitu adimu sana kama maji yalivyo adimu kwenye jiwe. Lakini unapoliona chozi hilo likitiririka, ujue kuna jambo limegusa sehemu ya ndani kabisa ya moyo wake.

Mwanaume anaweza kupita siku nyingi akiwa na mawazo mazito, akakutana na changamoto zinazomzidi nguvu, akapoteza matumaini mara kadhaa, lakini bado akaamka kila asubuhi na kuendelea kupambana kana kwamba hakuna kinachomsumbua. Wakati huohuo, kuna watu wanaomtegemea. Kuna familia inayomwangalia.

Lakini maisha hayamwulizi kama amechoka. Yanazidi kumpa mitihani.

Kuna usiku mwanaume anakaa peke yake, akitazama giza, huku mawazo yakizunguka kichwani mwake. Anajiuliza amekosea wapi, kwa nini anajitahidi lakini mambo ni zero.

Wakati mwingine chozi linamdondoka bila hata yeye kutarajia.

Kinachouma zaidi si kumwaga machozi, bali ni kumwaga machozi huku ukijua kwamba kesho bado unapaswa kuamka na kupambana na matatizo yaleyale.

Kama una simulizi yako, shiriki nasi. Huenda maneno yako yakawa faraja kwa mwanaume mwingine anayepitia vita ambayo hakuna anayeiona.
 
Hii imekuwa kama ndio petrol bila hivyo hatutoboi bila ugumu huwezi kuendelea
 
Wanaolia ni wale wanaoona urahisi wa maisha katika akili zao (imagination), wakipigwa ngumi kali na maisha ndipo hubenua midomo na kutokwa na machozi!
 
Screenshot_20261012-161229~2.jpg
 
Mara nyingi tu.Halafu kinacholiza zaidi ni kwamba hakuna anayekuja kukuokoa...Njia pekee ya kutulia ni kufa,nalo sio chaguo so unalia usiku mzima asubuhi unarudi kupambana kama sio wewe uliyelia jana...

Halafu ukitaka maisha yako yawe magumu zaidi jifanye unaweza kupambana huku unampenda mtoto wa mtu,mzee utalia mara mbili...
 
Hao waliozaliwa/kukulia katka familia zilizojipata hawawez kuelewa ulichokisema ila cc wenzangu na mim ndo tunajua joto lake, kikubwa ni kuamka unajipga kifua unasema "mim ni mwanaume nitapambana had tone la mwisho!"
 
Kama huzijui shida za maisha kaa utulie usome au rudi tiktok kupeleka muda usubiri chakula cha usiku kiive hapo kwa dada yako
Mkuu, nakuheshimu sana, lakini umenitukana kirejareja, nimevumilia.

Ok, kwani wewe huoni wanaume wakiteseka huku wake zao wakiwa wanakaa tu nyumbani kusubiria chochote kitu kitu Kwa waume zao?

Na wakati mwingine mke anapata pesa kwenye shughuli zake, lakini hatoi kwenye matumizi ya familia kwa sababu mmeshaaminishwa na hizo dini mnaona ninyi ndio viduma na mnapaswa kuhudumia tu!
 
Back
Top Bottom