Mwanaume, umewahi kufika mahali ukamwaga chozi kwa sababu ya ugumu wa maisha ?

Mwanaume, umewahi kufika mahali ukamwaga chozi kwa sababu ya ugumu wa maisha ?

Binafsi sijawahi, pamoja na changamoto kubwa ambazo nimewahi kupitia (not necessarily to write)

Huwa najifariji na msemo wa a better tomorrow is coming

Kwa kila jaribu lipo tumaini
 
Sijawai kumwaga chozi Mimi ila nimewahi kushindia andazi moja tu kwa siku nikajisemea moyoni haya ni mapito tu na kweli yamepita ila nimeshuhudia mtu mzima kunizidi Mimi akimwaga chozi..
Ohoo! Ukisikia mtu mzima analia ujue Kuna jambo!
 
Ishawahi kunikuta hii ,
Maisha ukiya tazama maisha yako kama vile hayana mwanga huna tumaini na wala huna mwanga nayo kabisa.

Ukiangalia kabisa huna uhakika na kesho yako kabisa

Leo tu ukicheki ni tatizo kila ukijaribu katika mambo yako mambo yana buma

Chozi zito lilinitoka nikaona kabisa haya maisha ni mapambano kati ya mimi na maisha.

Na siyo
Mungu,maisha na mimi.

Lakini baada ya kutokwa na machozi nakuwa najua kuwa

Maisha yangu ni yangu & tumaini langu ni mimi kuyabeba maisha yangu.

Ila nakuwa nimetoka na mafunzo makubwa na U serious wa maisha unakuwa umeongezeka zaidi.
 
Binafsi sina machozi ya kuchezea Ila Kwa mwendo huu wa uchumi wa kuchechemea kabla ya mvua za El Nino hazijaanza ,naziona kabisa dalili za kulia.
 
Chozi la mwanaume kwenye mapambano ya maisha ni kitu adimu sana kama maji yalivyo adimu kwenye jiwe. Lakini unapoliona chozi hilo likitiririka, ujue kuna jambo limegusa sehemu ya ndani kabisa ya moyo wake.

Mwanaume anaweza kupita siku nyingi akiwa na mawazo mazito, akakutana na changamoto zinazomzidi nguvu, akapoteza matumaini mara kadhaa, lakini bado akaamka kila asubuhi na kuendelea kupambana kana kwamba hakuna kinachomsumbua. Wakati huohuo, kuna watu wanaomtegemea. Kuna familia inayomwangalia.

Lakini maisha hayamwulizi kama amechoka. Yanazidi kumpa mitihani.

Kuna usiku mwanaume anakaa peke yake, akitazama giza, huku mawazo yakizunguka kichwani mwake. Anajiuliza amekosea wapi, kwa nini anajitahidi lakini mambo ni zero.

Wakati mwingine chozi linamdondoka bila hata yeye kutarajia.

Kinachouma zaidi si kumwaga machozi, bali ni kumwaga machozi huku ukijua kwamba kesho bado unapaswa kuamka na kupambana na matatizo yaleyale.

Kama una simulizi yako, shiriki nasi. Huenda maneno yako yakawa faraja kwa mwanaume mwingine anayepitia vita ambayo hakuna anayeiona.
 
Back
Top Bottom