Mwanaume, umewahi kufika mahali ukamwaga chozi kwa sababu ya ugumu wa maisha ?

Binafsi sijawahi, pamoja na changamoto kubwa ambazo nimewahi kupitia (not necessarily to write)

Huwa najifariji na msemo wa a better tomorrow is coming

Kwa kila jaribu lipo tumaini
 
Sijawai kumwaga chozi Mimi ila nimewahi kushindia andazi moja tu kwa siku nikajisemea moyoni haya ni mapito tu na kweli yamepita ila nimeshuhudia mtu mzima kunizidi Mimi akimwaga chozi..
Ohoo! Ukisikia mtu mzima analia ujue Kuna jambo!
 
Ishawahi kunikuta hii ,
Maisha ukiya tazama maisha yako kama vile hayana mwanga huna tumaini na wala huna mwanga nayo kabisa.

Ukiangalia kabisa huna uhakika na kesho yako kabisa

Leo tu ukicheki ni tatizo kila ukijaribu katika mambo yako mambo yana buma

Chozi zito lilinitoka nikaona kabisa haya maisha ni mapambano kati ya mimi na maisha.

Na siyo
Mungu,maisha na mimi.

Lakini baada ya kutokwa na machozi nakuwa najua kuwa

Maisha yangu ni yangu & tumaini langu ni mimi kuyabeba maisha yangu.

Ila nakuwa nimetoka na mafunzo makubwa na U serious wa maisha unakuwa umeongezeka zaidi.
 
Binafsi sina machozi ya kuchezea Ila Kwa mwendo huu wa uchumi wa kuchechemea kabla ya mvua za El Nino hazijaanza ,naziona kabisa dalili za kulia.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…