ni kweli kabisa, na tunavyoongea haya hapa jf wakina dada waliopo kwenye hii forum wanafikiria tunawalenga wao hawawazi kwamba hata sisi tuna ndugu wa kike pia.
Mimi kuna binti wa ndugu yangu mwaka huu alikua anaingia form 4, likizo ya mwisho wa mwaka jana alirudi nyumbani ana mimba. Alimtaja kijana mmoja ndio muhusika baada ya yule kijana kutafutwa aliikataa ile mimba. Alipewa lawama sana.
Wikiend moja nikamtafuta yule dogo alietajwa na binti kwamba ndio muhusika wa ile mimba. Nikaongea nae kirafiki tu kama kaka ake. Siwezi kusema kwamba sio mimba yake lakini alinifungukia mengi tu na mimi pia kama kaka nikampa nasaha zangu. Mpaka leo sijawahi kuchagua upande kwenye lile suala.
Tunalaumu sana wanaume lakini tunasahau kwamba hawa wanawake sio malaika
Kaka uzuri mimi na wewe ni miongoni mwa wachache tunaofahamu jinsi gani intersexual dynamics kwenye jamii yetu iliyobadilika, ambapo sasa hivi mgogoro wowote wa kimahusiano kati ya mwanamke na mwanaume jinsi unavyojadiliwa kihisia huku wengi wakichagua upande hasa wa mwanamke.
Siku hizi jamii inamuangalia mwanamke kama victim wa matendo ya mwanaume, chochote anacholalamika kuhusu mwanaume, wanaume na wanawake wanaungana kumshambulia mwanaume huyo anayelalamikiwa hata bila kujipa muda kuchimba undani wa jambo lenyewe.
Hali hii imepelekea wanawake kutake advantage ya huu ujinga wa jamii ya kuwaona wao innocent sana, na hivyo wanafanya mambo mengi sana ya kipuuzi kwa wanaume wakiamini kwamba jamii itakuwa upande wao.
Nina kisa kimoja cha jamaa alitalakiana na mke wake, huyo mshikaji alikuwa anatuma hela za matumizi ya watoto wao waliozaa na huyo mwanamke... sasa kumbe yule mwanamke zile hela alikuwa kiasi kidogo anatumia kwa watoto na kikubwa anatumia kwenye mambo yake binafsi, kuna kipindi watoto walikaa nyumbani miezi miwili bila kwenda shule, hadi ndugu zake na yule mwanamke wakauliza mbona watoto wapo tu nyumbani hawaendi shule..? alichojitetea yule mwanamke ni kwamba baba yao na wale watoto hajatuma ada ya kuwapeleka watoto shule, ikabidi wamtafute jamaa wamuulize, jamaa akasema mbona hela ya ada alishatuma siku nyingi sana na alimwambia kabisa kuwa hii ni hela ya ada, yule mwanamke akakaza uzi kuwa hajatumiwa ada.... aisee ikabidi wale ndugu zake waipeleke kesi ustawi wa jamii, kufika kule ustawi jamaa akaitwa kwanini hatoi ada ya watoto huku akishambuliwa sana na wale maafisa ustawi wa jamii.. jamaa hakutaka kujitetea kwa maneno akasema yeye ana uhakika pesa alishatuma na yuko tayari waende kwenye office za voda shop kuthibitisha hilo,.. basi bana kweli wakaenda huko voda shop na vielelezo vyote mpaka namba ya wakala, na kweli wakakuta jamaa alituma hela kitambo sana na ilipokelewa kwenye namba ile ile ya mwanamke, na hiyo pesa ilitolewa siku hiyo hiyo jamaa alivyomtuma.
Baada ya hapo ikawa ni aibu tupu kwa yule mwanamke na wale ndugu zake, wale maafisa ustawi wa jamii wakamgeukia tena mwanamke yule na kuanza kumshambulia, ndio ikabidi mwanamke yule afunguke sasa yote kwamba tangu watalakiane na jamaa maisha yake yamekuwa magumu sana, na amekujikuta akiingia kwenye madeni mengi na hata ile hela ya ada aliyotumiwa na jamaa aliitumia kupunguza madeni hili asidhalilike.
Sasa hebu angalia hiki kisa hapo awali kila mtu alikuwa anamlaumu na kumshambulia jamaa kwamba hajali watoto, wakati huo mwanamke akionekana ni innocent... imagine kama jamaa asingeomba waende kutafuta uthibitisho huko voda shop, kila mtu angebaki anamuona jamaa ni mtu wa ovyo sana na mwanamke pamoja na watoto angeendelea kuonekana ni victims wa ushenzi wa jamaa.
Na hivi ndivyo jamii yetu ya sasa ilivyo, once a woman is accusing you of any evil deed only hard irrefutable evidence can save you from public cynicism.
Wanawake wana take advantage ya ujinga wa jamii ya kisasa.