Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?


Tangu Ukabila ufutwe Mila nazo zimefutwa sijui kama unajua Hilo.

Watu Sasa wanaishi kisasa.
Katiba ya nchi ndîo Muongozo na siô Mila na desturi za Zamani za Makabila àmbayo Kwa Sasa hayana umuhimu wowote
 
Ni kweli, ila ujasema unakaa mda ukweni mkuu!

Kûna sababu za Mtu kukaa Ukweni kama zilivyo sababu za Mtu kukaa Nyumbani Kwao licha ya kuwa Mtu mzima.

Hivyo Muda WA kukaa inategemeana

Labda tujadili Kwa hoja Zenye mashiko. Unafikiri ni sababu zîpi kuu zinazokufanya uone Kukaa Ukweni NI JAU?
 
Tatizo ni wakwe zako, sasa sisi wakwe zetu poa sana, washikaji! Tunatinga kila mwaka, tena hadi likizo iishe!
 
Hongera zako! Ila sijajua jinsia yako mkuu
Mie mwanaume. Sasa mkwe wangu tuna biashara pamoja, na tunafanya mambo mengi pamoja. NI mwaminifu sana, na mchap kazi kweli kweli kwenye miradi tunayofanya pamoja. Sasa ukimfanya mkwe ni mtu wa kukuzalia mke tu, na ukawa na aina ya uhusiano ambao wewe ndio msaada kwa mkwe, unaongea nao mara moja moja wakimpigia simu mkeo na kusema tunaomba tumsalimu, utakaa huko ukweni kufanya nini? Make your inlaws part of your family, and be genuinely happy when you see them.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…