Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Poa mkuu umeeleweka
 
Ukishaoa pale pia ni nyumbani. Mfano umeoa tabora na unaishi dar inakuwaje?
Jitahidi ujenge kabanda kama unautaratibu wa kukaa sana ila kukaa ukweni zaidi ya siku moja lazima kuna mazoea ya ajabu yataanza tu... kama kuna tatizo au ishu ya msingi ambayo inawakutanisha watu wengi hapo sawa nawe unaweza kushiriki nao hadi watu wakianza kutawanyika na wewe aga sepa.
 
Kwetu kawauda hiyo, wakwe zetu wanaishi kwetu.

Kwanza sisi hatukubali kukaa kwa mume bila ya yeye kukaa kwetu.

Tukanyanyaswe?
 
Mila za watu wa pwani....
Kuna mahala nilishuhudia mtu ameoa na anaishi na mke wake huko huko ukweni
Kwa sisi tuliooa WACHAGA,

Suala la kulala ukweni ni MARUFUKU! Yaani SAHAU!

Kwanza binti akishaolewa, YEYE mwenyewe haruhusiwi kulala kwao, sembuse wewe??

Mimi alifariki baba mkwe, nililala lodge wiki nzima. Kila siku naenda msibani asubuhi, usiku narudi lodge kulala.
 
Dah wachaga mbona nasikia ni wabaguzi kama huna hela unaweza lala hata kwenye migomba hawana habari na wewe ni kweli?
 
Dah wachaga mbona nasikia ni wabaguzi kama huna hela unaweza lala hata kwenye migomba hawana habari na wewe ni kweli?
Mimi sijui kama ni ubaguzi au ni nini lakini utaratibu wao ndio uko hivyo. Mwanamke akishaolewa haruhusiwi kurudi nyumbani na kulala. Ataenda kusalimia tu asubuhi na kuondoka jioni kurudi kwa mumewe.

Na hii haijalishi hata kama mwanamke ameolewa nyumba ya 3 kutoka kwao, hawezi kwenda nyumbani kulala.

Binafsi niliona kama ni utaratibu mzuri
 
Yap utaratibu mzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…